Lil Wayne matatani, polisi walazimika kuvunja nyumba yake ya Miami kwa sababu hizi…

Msanii wa muziki wa HipHop Marekani, Lil Wayne amejikuta matatani baada ya polisi kuibuka nyumbani kwa msanii huyo na kuzuia baadhi ya mali zake ikiwa ni sehemu ya hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Miami siku ya Jumanne 03 November 2015.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, polisi hao walipewa ruhusa na Mahakama husika kufanya kitendo hicho baada ya rapper huyo kutoka New Orleans kushindwa kulipa gharama za ndege binafsi aliyoikodisha kwa mkataba na Miami Signature Group... mtandao huo umeendelea kusema kuwa, rapper huyo anadaiwa kiashi cha dola milion 2 ambazo ni zaidi ya bilion 4 za Kitanzania!
MIAMI WAYNE
Polisi hao walifika nyumbani kwa rapper huyo lakini wakazuiliwa na watu wa security getini, lakini polisi walitoa taarifa kuwa wameagizwa na Mahakama ya Miami kuzuia baadhi ya mali za msanii huyo baada ya yeye kushindwa kutekeleza wajibu wake wa kimkataba na kampuni ya Signature Group, kampuni inayojihusiha na biashara ya kukodisha ndege binafsi.
WAYNEMIAMI
Kufidia deni analodaiwa polisi hao walilazimika kuvunja milango ya nyumba ya msanii huyo na kuzuia baadhi ya mali zenye gharama kubwa ili kupata vitu vitakavyotosheleza fidia ya deni la kampuni hiyo, na wakati polisi wanafanya yote hayo Rapper huyo alikuwa hajulikani yupo wapi na wala alikuwa hapatikani kwenye simu zake za mkononi.
Unaweza pia ukaicheki video hii hapa chini kwa taarifa zaidi juu ya deni la Lil Wayne na kampuni hiyo ya ndege.
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.