KANU BALOZI MPYA WA STARTIMES BARANI AFRIKA
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa StarTimes nchini Naigeria, Bw. Jack Liu (wa pili
kulia) akiwa ameshikilia sare ya kampuni hiyo pamoja na mabalozi wapya
Jonathan Akpoborie (wa kwanza kushoto) na Kanu Nwankwo (katikati) wakati
wa hafla fupi ya kuwatambulisha mabalozi wapya wa kampuni hiyo jijini
Lagos Naigeria mwishoni mwa wiki. Wakijumuika kwa pamoja katika tukio
hilo ni wafanyakazi wa kampuni hiyo nchini Naijeria Bw. Maxwell Loko na
Dare kafar (wa kwanza kushoto).
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa StarTimes nchini Naigeria, Bw. Jack Liu (wa pili
kulia) akiwa ameshikilia sare ya kampuni hiyo pamoja na mabalozi wapya
Jonathan Akpoborie (wa kwanza kushoto) na Kanu Nwankwo (katikati) wakati
wa hafla fupi ya kuwatambulisha mabalozi wapya wa kampuni hiyo jijini
Lagos Naigeria mwishoni mwa wiki. Wakijumuika kwa pamoja katika tukio
hilo ni wafanyakazi wa kampuni hiyo nchini Naijeria Bw. Maxwell Loko na
Dare kafar (wa kwanza kushoto).
Na Mwandishi Wetu, Naigeria
Katika
kuhakikisha huduma za dijitali zinafurahiwa na zinamfikia kila mtu,
kampuni ya StarTimes imeingia makubaliano na aliyekuwa mchezaji nguli wa
kimataifa wa soka wa Naijeria, Nwankwo Kanu kama balozi wa shughuli
zake barani Afrika.
Akizungumzia
juu ya ushirikiano huo Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes nchini
Tanzania, Bw. Lanfang Liao amebainisha kuwa, “Mkataba baina yetu na Bw.
Kanu ulitiwa sahihi jijini Lagos nchini Naijeria ambako Bw. Kanu
alikubali kuingia mkataba kwa miaka mitatu. Hivyo basi balozi wetu huyu
mpya atakuwa muwakilishi wa kampuni yetu yenye shughuli zake takribani
nchi 12 barani Afrika zikiwemo Naijeria, Tanzania, Kenya, Uganda, Afrika
ya Kusini, Msumbiji, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na nyinginezo.”
Kwa
mujibu wa makubaliano ya mkataba huo, Kanu sasa atakuwa akishiriki
katika shughuli kama vile matangazo, kuhudhuria sherehe za kampuni,
matukio na kusaidia kukuza muonekano wa StarTimes barani Afrika pamoja
na hamasa kwa watu kuhamia katika mfumo wa dijitali.
Kanu
pia atakuwa akisaidiana na aliyekuwa mchezaji wa kimataifa wa soka wa
Naijeria, Bw. Jonathan Akpoborie ambaye yeye pia ameteuliwa kuwa
mtaalamu wa kupanga vipindi vya michezo na mgeni mulikwa katika
uchambuzi wa vipindi vya moja kwa moja. Bw. Akpoborie atakuwa akishiriki
kama mchambuzi wa kiufundi wa vipindi vya moja kwa moja vya michezo
vitakavyokuwa vikirushwa katika chaneli za StarTimes vikionyesha
uchambuzi na makala yakinifu.
Bw.
Jonathan Akpoborie ni mchezaji wa zamani wa kimataifa kutoka nchini
Naijeria ambaye alitumia muda wake mwingi kucheza soka la kulipwa nchini
Ujerumani.
Akifafanua
umuhimu wa kumchagua Bw. Nwankwo Kanu kama balozi wa StarTimes Afrika,
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu huyo nchini Tanzania amesema kuwa StarTimes
ilizingatia sana la mtu ambaye anakaubalika si tu nchini mwake bali
katika bara zima la Afrika.
“Ukiachilia
mbali mafanikio aliyoyapata Kanu katika medali za kimatifa, umaarufu
wake haupo tu nchini kwake Naijeria bali katika bara zima la Afrika.
Kanu ni hamasa ya kweli katika historia ya mafanikio ya wanasoka kutoka
Afrika kwa kufikia mafanikio makubwa licha ya mazingira magumu. Ni mfano
wa kuigwa ambaye kila mtu anaweza kumtazamia kufikia ndoto zake.”
Alisema Bw. Liao
Aliongezea
pia, “Wakati dunia tayari imekwishahama kutoka kwenye mfumo wa
analogia, StarTimes inawekeza vya kutosha, kukusanya rasilimali na
kuwahusisha wadau ili kuhakikisha waafrika wanaingia katika mfumo mpya
wa matangazo ya luninga kwa dijitali na kuwaunganisha na ulimwengu kwa
ujumla. Tunapigania kuwaunganisha watu wengi zaidi, kuwahamasisha na
kuwapatia msisimko wateja wetu kote barani Afrika kuhusiana na matangazo
ya dijitali.”
Naye
kwa upande wake akiwa mwenye furaha Bw. Nwankwo Kanu aliishukuru
kampuni ya StarTimes kwa kumuona anastahili kuwa balozi wa kampuni hiyo.
“Ninayo
furaha kubwa sana kusaidia kukuza na kuunga mkono shughuli za StarTimes
kama balozi wake barani Afrika. Lengo langu ni kuhakikisha kila
mwafrika amekuwa amehamia katika matangazo ya dijitali ifikapo mwezi
Juni 17, 2017 na nimefurahi kushirikiana na StarTimes katika
kulifanikisha hili.” Alisema Bw. Kanu
“Ukiachana
na kuwa kapteni mstaafu wa kikosi cha Super Eagles cha Naijeria, Kanu
ni mchezaji wa kiafrika mwenye mafanikio lukuki yakiwemo, kushinda
medali ya EUFA Kilabu Bingwa barani Ulaya, medali ya kombe la UEFA,
medali tatu za washindi wa kombe la FA na tunzo mbili za mchezaji bora
barani Afrika hizo zikiwa chache tu zilizoorodheshwa. Pia ni mchezaji wa
kipekee kuchezea soka la ligi ya Uingereza kushinda vikombe vya EUFA
Kilabu Bingwa barani Ulaya, kombe la UEFA, ligi kuu Uingereza, kombe la
FA na medali ya dhahabu ya Olimpiki.” Alihitimisha Bw. Liao
Kanu
pia atakuwa akishiriki kwenye uchambuzi wa kina pamoja na wapenzi wa
soka kama mgeni rasmi katika matangazo ya moja kwa moja ya mechi za ligi
za Bundesliga na Serie A zinazorushwa mahususi katika chaneli za
StarTimes.
StarTimes
kwa sasa inayo hakimiliki za kurusha moja kwa moja mechi za ligi za
Bundesliga (Ujerumani), Serie A (Italia) na Ligue 1 (Ufaransa). Na kwa
sasa inarusha moja kwa moja michuano ya FIFA kombe la dunia la vijana
chini ya miaka 17 iliyoanza kutimua vumbi Oktoba 18 na kumalizika
Novemba 8 nchini Chile.