Hiki ndicho kikosi cha Uganda kitakachopambana na Tanzania kesho


Timu ya taifa ya Uganda
Timu ya taifa ya Uganda
Viongozi kadhaa pamoja na wachezaji wa timu ya taifa ya Uganda wamewasili salama visiwani Zanzibar leo jioni na ndege ya shirika la Ethiopia tayari kwa mchezo wao wa kesho dhidi ya Tanzania ambao utafanyika kwenye uwanja wa Amani visiwani humo.
Mchezo huo niwa raundi ya kwanza ya mashindano ya mataifa ya Afrika yanayoshirikisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani.
Wachezaji wanaounda kikosi cha timu hiyo ni:
Walinda mlango: Alitho James, Bwete Brian
Mabeki: Hassan Wasswa (Nahodha), Denis Okoth, Brian Ochwo, Shafik Bakaki,  Deus Bukenya, Derrick Tekkwo
Viungo: Yasser Mugerwa, Kizito Keziron,  Erisa Sekisambu, Muzamiru Mutyaba, Farouk Miya, Martin Kizza
Washambuliaji: John Semazi, Frank Kalanda, Ssentongo Robert, Fahad Muhamed Hassan
Viongozi walioambatana na timu hiyo ni:
Dr. Bernard Patrick Ogwel [Kiongozi wa kamati ya ufundi ]
Sredojevic ‘Micho’ Milutin [Kocha mkuu]
Moses Basena [Kocha msaidizi]
Fred Kajoba [Kocha wa walinda mlango]
Herbert Nsubuga [Afisa uhusiano]
Ronald Kisolo [Dactari wa timu]
Joseph Mutaka [Afisa habari]
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.