HATIMA YA MESSY KUBAKI SIMBA NI LEO>>SOMA HAPA MAAMUZI YA TFF
\SHIRIKISHO
la kandanda Tanzania, TFF leo linawakutanisha Simba na mshambuliaji
wake, Ramadhan Singano 'Messi' kujadili utata wa mkataba uliopo baina ya
pande hizo mbili.
Singano
anadai ana mkataba wa miaka miwili aliosaini Mei mosi, 2013 na unatakiwa
kumalizika Julai 1, 2015, wakati Simba inadai Messi ana mkataba wa
miaka mitatu aliotia saini Mei 1, 2013 na unatakiwa kumalizika Julai 1,
2016.
Kutokana na utata huo, inaonekana kuna upande umechakachua mkataba na leo kinaweza kueleweka.
Juni 5
mwaka huu, TFF ilitangaza kumepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za
mgogoro wa kimkataba kati ya Mchezaji Ramadhani Singano na klabu ya
Simba.
TFF
ikaagiza mwakilishi wa klabu ya Simba pamoja na mchezaji wa Ramadhani
Singano wafike ofisi za TFF siku ya Jumanne tarehe 09/06/2015 kwa
mazungumzo na Kila upande umetakiwa kwenda na vielelezo vyake.
"Katika
kipindi hiki cha kuelekea kwenye mazungumzo,TFF inaziasa pande zote
mbili zijiepushe na kutoa matamko yanayoweza kuchochea hali ya
kutoelewana na kuamsha hisia mbaya katika familia ya mpira wa Miguu
Tanzania". Alisema sehemu ya taarifa ya TFF.(VICTOR)