Mapigano makali yaendelea Yemen
Mapigano
yameendelea katika mji wa Aden wa pili kwa ukubwa nchini Yemen, wakati
waasi wa Houthi wakijaribu kutwaa udhibiti wa mji huo kutoka kwa
wanamgambo wa eneo hilo.
Watu
walioshuhudia tukio hilo mjini Aden wameripoti kutokea kwa mashambulio
makali ya waasi, kuwepo kwa waasi walenga shabaha wakiwa juu ya mapaa ya
nyumba na maiti kuzagaa mitaani.
Kuna
wasiwasi wa kuongezeka kwa idadi ya watu waliojeruhiwa wakati waasi
wakiendelea kusonga mbele licha ya mashambulio ya anga kufanyika kwa
zaidi ya wiki moja dhidi ya majeshi ya Houthi kutoka majeshi ya
washirika yanayoongozwa na Saudi Arabia.
Msemaji
wa majeshi ya washirika, Ahmed Asiri, amethibitisha kuwepo mapigano
makali."Sasa wanashirikiana, serikali ya mseto na jeshi la Yemen
kuwazuia wapiganaji wa Houthis kudhibiti mji wa Aden. Kwa kweli hawana
misaada inayoingia Aden. Majeshi yaliyokuwa yamejificha mjini Aden sasa
yanasonga mbele na kuelekea Shabwa. Tunaendelea kufanya kazi kuhakikisha
kuwa Aden unasafishwa haraka na kuwa salama kwa utawala wa serikali
halali
Msemaji
wa shirika la misaada la Medecins sans Frontieres ameiambia BBC kuwa
hospitali ya shirika hilo mjini Aden imepokea zaidi ya majeruhi 500
kutoka pande zote za mgogoro katika kipindi cha wiki mbili zilizopita.
Jeshi la Saudi Arabia limesema katika mashambulio ya hivi karibuni,
walikiharibu kikosi cha jeshi la majeshi ya Yemen chenye kushirikiana na
waasi.(BBC)