MAMA AWAFUNGIA NDANI WATOTO WAKE 3 KWA MIAKA 10 HUKO MAFIA!
Katika
Kisiwa cha Mafia mkoa wa Pwani mama aitwaye Mwasiti Ally amekuwa
akiwafungia ndani watoto wake ndani kwa muda wa miaka 10 sasa kwa madai
kuwa ni wagonjwa wa akili.
Watoto
hao huko ndani ya chumba wote wamebadilika na kuwa na afya mbaya huku
kucha za mikononi na miguuni kurefuka sana, nywele zimekua ndefu kiasi
cha kutisha na sura zao kuonekana kama za misukule na kuwa kama walemavu wa miguu.
Alianza
kuugua mtoto mmoja ambaye ni wa kwanza kuzaliwa, cha ajabu, kila mwaka
mwingine akafuatia hadi wa tatu. Mama huyo anadai Sababu kubwa ya
kuwafungia ndani tangu mwaka 2005 anasema ni kwaajili ya usalama wao
maana anaamini kwa kuwaachia tu wangeweza hata kupotea.
