MWANAMKE HUYU ASHIKA MIMBA MARA MBILI NA KUZAA WATOTO WANNE NDANI YA MWAKA MMOJA.!! IKO HAPA
Tuliwahi
kuandika stori ya mwanamke kujifungua watoto mapacha ambao walipishana
miezi miwili waliozaliwa katika moja ya hospitali huko Romania na
kuonekana kugusa hisia za watu wengi.
Hii
tena imetokea huko Uingereza baada ya mama mmoja kupata watoto wanne
ikiwa ni matokeo ya kushika ujauzito mara mbili ndani ya mwaka mmoja.
Sarah Ward mwenye umri wa miaka 29 alipata mapacha watatu ikiwa ni mwezi mmoja tangu ajifungue mtoto wake wa kwanza wa kiume,
Mwanamke
huyo alijifungua mapacha hao watatu ambao walizaliwa kabla ya muda huku
mtoto wake wa kwanza akiwa tayari na miezi nane.
Sarah
amesema anashukuru kupata watoto hao na amekua akitumia nepi zaidi ya
30 kwa siku kwa ajili ya kuwabadilisha watoto wake lakini haoni kama ni
gharama kutokana na furaha aliyonayo.
Alisema
alipata wakati mgumu wakati akijaribu kushika mimba ya mtoto wake wa
kwanza na madaktari walipogundua ana mimba ya watoto mapacha watatu
walimshauri kumtoa mmoja ili watakaosalia waweze kukua vizuri lakini
alikataa na kutaka waache wote.