MSIGWA, LISSU, LEMA NA PROFESA J KUTIKISA IRINGA MCHANA WA LEO
![]() |
WAKATI
Chama cha Mapinduzi (CCM) kikitarajiwa kufanya mkutano wake mkubwa
kesho jumapili katika viwanja vya Mwembetogwa mjini Iringa, Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) leo Jumamosi kinatarajiwa kufanya
kufuru katika uwanja huo huo.
Mkutano
huo ulioandaliwa na Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) unatarajiwa
kuwashirikisha viongozi mbalimbali vinara wa chama hicho.
Mbali
na Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, wengine
wanaotarajiwa kuhutubia katika mkutano huo ambao maandalizi yake
yamekwishakamilika ni pamoja na Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu
ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, Mbunge wa Arusha Godbless
Lema na Msanii wa kizazi kipya ambaye hivikaribuni ametangaza nia ya
kuwania ubunge katika jimbo la Mikumi, Profesa J.
Tofauti
na mikutano mingi ambayo kimekuwa kikifanya mjini hapa, safari hii,
labda kutokana na ujumbe mzito, chama hicho kitatumia jukwaa la kisasa
ambalo halina tofauti na majukwaa yanayotumiwa katika shughuli kubwa za
kisanii nchini.
Leo
na kesho wakazi wa Iringa wanatarajia kusikiliza sera za vyama hivyo
vya Chadema na CCM ikiwa imebaki miezi michache kabla ya kufanyika kwa
Uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani.
