Mikataba ya Owino, Ndemla yafutwa Yanga, Msuva stop
Mikataba ya Owino, Ndemla yafutwa Yanga, Msuva stop
KOCHA wa
Yanga, Hans Pluijm, ambaye ni miongoni mwa makocha wachache wenye
misimamo kwenye Ligi Kuu Bara, ameapa kwamba ndani ya mkataba wake na
Yanga, si Said Ndemla, Joseph Owino, Ivo Mapunda, Haroun Chanongo, Amri
Kiemba wala Shabaan Kisiga hakuna atakayevaa jezi ya Yanga.
Wachezaji
hao sita wanamaliza mikataba yao na Simba msimu huu na mpaka sasa
hawajaongezewa huku viongozi wa Mnyama wakihofia kwamba Yanga inaweza
kuwatia kitanzi muda wowote mastaa wao wawili; Owino na Ndemla.
Kocha
huyo ambaye viongozi wa Yanga wametokea kumwamini sana amesisitiza
kwamba pia hataruhusu kiungo mshambuliaji wao, Simon Msuva kusajiliwa na
Wekundu wa Msimbazi.
"Msuva
namjua vyema kuliko mashabiki wanavyomjua najua umuhimu wake, lakini pia
najua mapungufu yake ukiangalia yanazidi kupungua muda unavyozidi
kwenda,ni mchezaji anayehitajika hapa Yanga ni vyema sasa mashabiki
wakamuacha acheze aisaidie timu, nikiwa hapa Yanga siwezi kufanya kosa
la kumuacha aondoke hasa kwenda Simbam," alisema.(P.T)
"Nimepanga
jambo moja nikiwa kocha wa Yanga, sitasajili mchezaji yeyote kutoka
Simba hata awe na ubora kama Lionel Messi wa Barcelona, nimegundua jambo
moja hata wakija hapa hawaaminiki na watu wa Yanga ni vyema tukasajili
kutoka timu zingine lakini sitasajili kutoka Simba."
Kauli
hiyo ya kocha huyo amezima ndoto za mastaa hao wa Simba kupewa mikataba
na Yanga kwani hata uongozi wa juu umeonywa na wanachama kwamba
wasisajili mtu yeyote kutoka Simba kwa vile hawana msaada na wanafanya
Yanga inakuwa mteja kwa Simba kila wanavyokutana katika mechi zao.
Wanachama
matajiri wa Yanga wamekuwa na tabia ya kununua wachezaji mahiri wa
Simba kila inapofika mwisho wa msimu ili kudhohofisha wapinzani wao,
lakini hali hiyo huenda mwaka huu ikashindikana mpaka mkataba wa Pluijm
utakapomalizika mwishoni mwa mwaka ujao na hata ukimalizika huenda
akaongezwa kama ufanisi wake ukiimarika.
Katika
hatua nyingine, Yanga juzi Jumammosi walitumia Sh5 milioni ndani ya saa
tatu kuwanunulia viatu maalumu wachezaji kwenye mechi dhidi ya Mgambo
JKT iliyopigwa Tanga na Yanga kushinda mabao 2-0.
Hiyo ilitokana na Uwanja wa Mkwakwani,Tanga kujaa matope kufuatia mvua kubwa iliyonyesha siku moja kabla ya mechi hiyo.
Wakiongozwa
na Mwenyekiti wa Kamati ya mashindano, Mhandisi Isaac Chanji, ambaye
aliambatana na mjumbe wake katika kamati hiyo, Yusuphed Mhandeni na
Katibu wa timu hiyo Dk. Jonas Tiboroha, mabosi hao walilazimika kutumia
kiasi hicho kununua viatu hivyo maalumu ambavyo vilitumiwa na wachezaji
kupata ushindi huo muhimu.
"Kweli
walinunuliwa viatu, isingekuwa rahisi kupambana na viatu vya kawaida
katika uwanja kama ule, lakini sio wote waliovitumia kuna wengine
walitumia vyao," alisema Pluijm.
Chanzo:Mwanaspoti