AHUKUMIWA MIAKA 20 JELA KWA KOSA LA KUMUOA DADA YAKE ALBINO HUKO KAHAMA
Mahakama
ya wilaya ya kahama mkoani Shinyanga Jana imemuhukumu kwenda jela miaka
20 Ally Sanyiwa (24) kwa kosa la kumuoa dada yake Mektilda Sanyiwa(20)
mkazi wa Chela.
Imedaiwa
mahakamani hapo na mwendesha mashitaka wa polisi Koplo Evodia mbele ya
hakimu mfawidhi George Mariki kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo
mwezi machi mwaka huu.
Aidha
koplo Evodia ameiambia mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa huyo aliweza
kumtorosha dada yake na kisha kumpeleka katika kijiji cha Mazimba na
kuishi naye.
Wazazi
wa Mektida ambaye ni mlemavu wa ngozi (albino) wamesema kuwa mara baada
ya binti yao kutoweka nyumbani walipata hofu na kuanza kumtafuta mpaka
alipopatikana akiwa anaishi nyumba moja na kijana wao.
Mahakama
hiyo imetoa hukumu kwa mtuhumiwa huyo mara baada ya kukiri kutenda kosa
hilo ambalo ni kinyume na maadili ya kitanzania.