L Enrique:El Classico haitaamua mshindi
L Enrique:El Classico haitaamua mshindi
Kocha wa Barcelona Luis Enrique
Kocha wa
Barcelona Luis Enrique amesema kuwa mchuano wa jumapili kati ya
wapinzani wakuu katika ligi ya La Liga, Real Madrid na Barcelona
haitaamua ni nani atakayeshinda ligi.
Huku ikiwa takriban mechi 11 zimechezwa ,kilabu ya Barcelona iko mbele na pointi moja dhidi ya Real Madrid.
Messi na Ronaldo
''Ni
mechi muhimu lakini sio itakayotoa mshindi wa ligi ,alisema Enrique
ambaye aliwahi kuzichezea timu zote mbili.Mechi hizi huwa tofauti sana
ukilinganisha na nyengine,ni mahasimu wetu wa jadi .Pia kuna tofauti ya
mabao yaliofungwa katika ya timu hizi mbili.Hakuna mshindi wa moja kwa
moja anayepigiwa upato wakati wa mechi kama hizi,lakini tunapocheza
mbele ya mashabiki wetu sisi hupata motisha zaidi''.alijigamba Luis
Enrique.
''Hii ni fursa nzuri ya kuongeza pengo dogo lililopo kati yetu na Real Madrid''.aliongezea kocha huyo.BBC