AZAM FC: HATUJAMZUIA KAVUMBAGU KWENDA BURUNDI
Didier Kavumbagu
Uongozi
wa Azam FC umesema haujamzuia mshambuliaji wake wa kimataifa, Didier
Kavumbagu kurejea kwao kuitumikia timu yake ya taifa ‘Entamba
Murugamba’.
Jaffar
Idd Maganga, msemaji wa Azam FC, ameuambia mtandao huu kuwa Kavumbagu
yuko Tanzania kwa sababu ya uzembe wa Shirikikisho la Soka Burundi.
Amesema
kuwa shirikisho hilo liliwasiliana na uongozi wa Azam FC likimuomba
Kavumbagu kwa ajili ya kuitumikia timu yake ya taifa katika mechi ya
kirafiki ya kalenda ya FIFA mwishoni mwa wiki hili tangu wakiwa
Khartoum, Sudan wakicheza dhidi ya El-Merrikh, lakini mkali huyo wa
mabao amekwama kwenda kutokana na kutotumiwa tiketi ya ndege.
“Tumeshangazwa
na taarifa zinazoenezwa kwamba tumemzuia Kavumbagu kwenda kuitumikia
timu yake ya taifa. Hii tunaona imelenga kutuchafua kimataifa.
“Tulipata
taarifa za Kavumbagu kutakiwa na timu yake ya taifa tukiwa Sudan,
lakini ameshindwa kwenda kwa sababu hajatumiwa tiketi.
“Mchezaji anaruhusiwa na klabu yake kwenda kuitumikia timu ya taifa pale shirikisho linapokuwa limetuma tiketi kwa klabu husika. Tiketi ya Kavumbagu kwenda kuitumikia timu yake ya taifa si jukumu la Azam FC,” amesema Maganga.
“Mchezaji anaruhusiwa na klabu yake kwenda kuitumikia timu ya taifa pale shirikisho linapokuwa limetuma tiketi kwa klabu husika. Tiketi ya Kavumbagu kwenda kuitumikia timu yake ya taifa si jukumu la Azam FC,” amesema Maganga.
Kavumbagu,
mchezaji wa zamani wa Atletico FC ya Burundi na Yanga SC, ameifungia
Azam FC mabao 10 katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu ikiwa ni bao
moja nyuma ya kinara, Simon Msuva wa Yanga SC.(AI)