YANGA YAPOTEZA MUELEKEO WA SIMBA BAADA YA KUCHUKUA POINT 6 MBEYA
Vinara
wa ligi kuu ya vodacom Yanga wamefanikiwa kuvuna pointi 6 na magoli 6
katika uwanja wa sokoine ndani ya siku 4, baada ya leo kuwafunga Mbeya
City goli 3-1.
Yanga SC walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli moja bila, goli lililofungwa na Saimon Msuva akiunga mpira wa aruna Niyonzima katika robo ya kwanza ya mchezo.
Katika kipindi cha kwanza Mbeya city walicheza vyema eneo la kati ya uwanja lakini waka kosa mbinu ya kuipita ngome ya yanga iliyokuwa inaongozwa na nahodha Nadir aroub Cannavaro.
Katika dakika ya 54 Mrisho Ngassa aliiandikia goli la pili anga kufuatia makosa ya goli kipa David Baruani alipotaka kujaribu kumpiga chenga Ngassa baada ya kupoke mpira wa kurejeshewa.
Katika dakika ya 62 Mbeya city walifanikiwa kuandika goli la kufutia machozi, ikiwa ni goli la kwanza kufungwa kwa kipa Ally Mustapha Bateth katika michezo ya ligi kuu ya vodacom.
Hamisi Tambwe aliiandikia yanga goli la tatu katika dakika ya 72 na kupelekea mchezo kumalizika kwa yanga sc kushinda goli 3-1.
Katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Kambarage umeshuhudia Simba SC wakilala kwa goli 1-0 toka kwa Stand united na kupelekea Stand united kufikisha point 18 baada ya micheo 16 waliyo cheza.
Katika mchezo huo ulishuhudia wachezaji wawili wa stand united wakipewa kadi nyekundu katika dakika za lala salama.