The site for daily Tanzania Hard News and Entertainment
Home/Love/Wanawake Tuache Tabia ya Kuwaachia kila kazi Wafanyakazi waNdani..Mtasaidiwa Mpaka Kitandani..Soma Kisa Hichi
Wanawake Tuache Tabia ya Kuwaachia kila kazi Wafanyakazi waNdani..Mtasaidiwa Mpaka Kitandani..Soma Kisa Hichi
MUME: Darling nina kikao mkoani kesho naomba niandalie vitu please. MKE: Dada zile nguo za baba pamoja na soksi ulifua.
DADA:Ndio
nimepanga kabatini. mama anarudi chumbani na kumuomba hubby wakacheki
TV sebulen, lakini baada ya muda mama anamuita dada akapange suruali
kadhaa na mashati kwa ajili ya safari ya kesho, dada anapanga kila kitu
anatoka
MKE: Kama tayari hakikisha unarekebisha yale mashuka
pale kitandan weka na maji bafuni, dada anafanya na kwenda zake kulala,
asubuhi dada anaamka mapema na kuandaa kila kitu ikiwamo na chai,
babaanakunywa chai na kutaka kuondoka. MKE: Dada msindikize baba ili ufunge geti sbb bado ni giza.
DADA:
Sawa mama, dada anatoka na begi la baba hadi nje kwavile mkewe yupo
ndani , baba anamtaka dada abaki vizuri na watoto, dada anaitika na
kusema nawao wanamuombea safari njema. Baada ya muda baba anarudi toka
safari MKE: Huku akitabasamu, dada si umemuona baba amerudi vipi chakula tayari. DADA: Ndio. MKE:
Haya kapange meza vizuri mimi nandaa juice. Baada ya muda wanakula
nababa anagundua juice sio nzuri anaamua kuiacha na kusema leo wamesahau
kuweka baadhi ya vitu hivyo hataweza kuinywa.Baadae baba anakumbuka
kuwa aliacha boxer zake kwenye ndoo ya maji chumbanna kufunika mfuniko,
anamuuliza mama vipi zile nguo zangu kwenye ndoo zilifuliwa maana
nilisahau kusema kama zina maji. MKe: Dada njoo hapa hivi zile nguo za baba chumbani ulifua.
DADA: Ndio mama lakini hasemi kama alianua na kuweka chumbani kwake akidhan atakunja baada ya kazi kupungua MKE: Darling zilifuliwa. MUME: Na watoto vipi wameshalala. MKE: Anajibu wamelala darling. MUME: vipi dereva wao alifika kuchukua pesa yake.
MKE:Dada eti uncle Hassan amechukua pesa yake.
DADA:Hapana wamembadilishia gari uncle Hassan amesafiri kwa muda. MKE:Tutampatia darling siku akirudi acha dada aendelee kuitunza.
MUME: Basi vizuri, ehee vipi na tution walienda leo. MKE: Ndio walienda anamgeukia dada, si eti ee walienda si eti. DADA:Hapana Kelvin anaumwa leo siku yapili nilinunua dawa dukan nimempa lkn hajambo
MKE:Anashangaa
hee mtoto mgumu huyukumbe jana alikua mgonjwa halafu wala!!! alikua
anacheza tu jamani watoto,asante dada umefanya vizuri.
MUME: Haya mimi niwaache nataka nikapumzike lkn darl nitaomba zile boxer nichome kabla ya kulala sababu zimeanzakuchoka
MKE:
Anaingia chumbani anafungua kabati na kuzikosa lkn kabla hajajieleza
anamuona dada analeta mzigo wa boxer zikiwemo chupi za mama na mataulo.
MUME:
Basi dada zirudishe tutachambua kesho nenda kafanye kazi zako, mume
anainuka na kuelekea kulala, lakini anagundua mke wake alimwaga nguo
kitandani wakati anatafuta boxer hivyo anaamua kurudi sebuleni ili
aombe. kuandaliwa kitanda, kwavile chumba cha dada kipo jiran na chao
anagundua dada ameacha mlango wazi.Anaamua kuufunga ili mbu wasiingie
lakini anaona baadhi ya mashati na suruali zake zikiwa zimenyooshwa na
kuwekwa pemben huku kitanda kikiwa kimetandikwa kwa ustadi anaamua
kufunga mlango na kutoka, anafika sebuleni anakuta mama anatazama
tamthilia anamwambia akatandike kitanda. MKE: Dada njoo, (kwa sauti ya kunong'ona) naomba ukatandike kitanda haraka. DADA:Tayari nilipeleka viatu vya baba nikaamua kutoa na zile nguo.
MKE: anaamka na kwenda kuhakikisha anarudi na kumwambia mumewe tayari aende akalale
MUME:
anaenda kulala lkn huku akijuiliza sana ni nini amfanyie huyu dada kwa
ukarimu anaowafanyia hapo nyumban, kwanza anajua ni vitu gani baba
anabeba akiwa safarini, ndio pekee anaemtakia safari njema na kumuombea,
ndio anaefuaboxer zake na kutunza vizuri, ndio anaepika chakula
kitamu, ndio anaetandika kitanda chake, ndio anaejua juice gani baba
anapenda, ndio anaejua kama watoto wamerudi vipi kutoka shule, vilevile
ndio anaejua kama watoto wake wanaumwa ama vipi.Sasa mnafikiri baba
atamzawadia nini huyu binti ambae amebakiza kujua style anazopenda baba
tu, si atamfundisha ili kesho asimsumbue tena mke wake ambae kila kitu
lzm amuulize dada.Akina baba hawaridhiki lakini wamama jitahidini hata
kama mnamajukumu kiasi gani.