Posho Mpya Yanga Kufuru ni Kama TP Mazembe, Simba na Azam Azioni Ndani

NEEMA imewadia kwa wachezaji wa Yanga baada ya uongozi wao kutangaza kwamba kuanzia sasa posho zote juu, tena si posho tu bali wanafikiria pia kuongeza motisha nyingine kama mabao yanayofungwa, pasi za mwisho na kujituma zaidi kwa mchezaji binafsi.

Posho hizo zitakuwa kubwa kuliko zile wanazopewa wachezaji wa Simba hata klabu tajiri ya Azam FC. Kwa mujibu wa uongozi ni kwamba posho za wachezaji wake kwenye mechi za Ligi Kuu Bara zitaongezeka mara mbili ya kiwango cha sasa. Mtendaji Mkuu wa Yanga ambaye ni Katibu, Jonas Tiboroha ameliambia Mwanaspoti kuwa wamefanya marekebisho ya posho hizo ili kuwaongezea wachezaji wao motisha ya kufanya vizuri katika mechi za ligi na kufanikiwa kutwaa taji hilo kwa mara ya 25.
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.