NYUMBA ZAUNGUA KWA MOTO WA AJABU HUKO MOROGORO, WANANCHI WALALA NJE SIKU 7 MFULULIZO... HOFU YA UCHAWI YATAWALA
Katika hali isiyo kuwa ya kawaida familia tatu zenye watu 16 katika kijiji cha Mikese mkoani Morogoro wanalazimika kulala nje kwa siku saba mfululizo baada ya nyumba wanazoishi kuwaka moto mara kwa mara na kuunguza samani za ndani na vyakula.
Inaelezwa kuwa chanzo cha moto huo hakifamahamiki na hivyo kusababisha hofu kwa familia hizo kutaka kuyakimbia makazi yao.
Mwandishi
wa habari hizi amefika katika familia hizo na kuona vitu mbalimbali
vilivyoungua moto vikiwemo vyakula nguo madaftari ya wanafunzi huku
wakinamama na watoto pamoja na wazee wakiwa nje.
Wananchi
hao wamesema katika hali isiyokuwa ya kawaidia moto huo huwaka zaidi
ya mara tisa kwa siku na wanajaribu kuuzima lakini chanzo cha moto huo
hakieleweki ingawa nyumba hizo hazina umeme wala nishati ya aina yoyote
inayosabaisha moto.
Wananchi
hao wamefananisha tukio hilo kama la miujiza na kuomba watu wenye
imani mbambali kufika na kufanya maombi katika nyumba hizo kwani
wanateseka kwa kushindwa kulala ndani.
Mwenyekiti
wa serikali ya kitongoji cha Lukole Ramadhani Shaban amekiri kuwepo
kwa matukio ya moto kuwaka katika nyumba hizo kwa siku saba mfululizo.
Amesema
siyo tukio la kawaida na jitihada wanazozifanya kama serikali ya
kijiji wameanza kuwatafuta wachungaji na mashekhe ili kusaidia
kufanya maombi katika nyumba hizo kwani familia hizo zinaishi katika
mazingira magumu ya kulala nje kwa muda mrefu.
Via>>Itv
Via>>Itv