NAIBU WAZIRI WA MAJI AMOS MAKALLA ATUMIA BODABODA KUFANYA ZIARA JIMBONI KWAKE
Msafara
wa Mbunge wa Jimbo la Mvomero na Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla
kuelekea kitongoji cha Ifumbo kilicho kilomita 20 toka kijiji cha
Mvomero.
Mbunge
wa Jimbo la Mvomero na Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla akiwa
amepakiwa kwenye pikipiki (Bodaboda) wakati akielekea kwenye kitongoji
cha Ifumbo kilicho kilomita 20 toka kijiji cha Mvomero.
Mbunge
wa Jimbo la Mvomero na Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla jana
alifanya ziara katika Jimbo lake hilo kwa kutumia usafiri wa pikipiki
kufika kitongoji cha Ifumbo kilicho kilomita 20 toka kijiji cha Mvomero
ambacho kwa historia hakijawahi kufikiwa na kiongozi yeyote tangu uhuru.
Mbunge
huyo ambaye amesifika na kuweka rekodi ya kutembelea vijiji vyote 130
vya Jimbo lake hilo,aliona umuhimu kuwafikia wananchi na wana CCM wa
Ifumbo kwa njia ya pikipiki ili ajionee changamoto na kuchukua hatua
stahiki ili kukabiliana nazo.
Makalla
alifika kwenye kitongoji hicho cha Ifumba na kulakiwa kwa shangwe na
wananchi wa kijiji hicho ambao walifurika kwa wingi kumpokea, na
amehaidi kutuma watalaam wa halmashauri wafike na kuiona barabara na
kuingiza katika mipango.
Aidha
alikagua ujenzi wa shule ya msingi Ifumbo na kuchangia mifuko 100 ya
saruji kwa ajili ya maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo,pia amesaidia timu
ya Ifumbo Star jezi na mpira na kuwahamasisha kujiandikisha kwenye
daftari la wapigakura pindi litakapoanza.