AMKATA MPWA WAKE SEHEMU ZA SIRI -TUNDURU
MKAZI
wa Kijiji cha Majimaji kilichopo Tunduru mkoani Ruvuma, Patrick Vitus
(70), amekatwa sehemu zake za siri na kuachwa zikining’inia.
Akizungumza
Jumamosi kwa njia ya simu jana, Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho, Hussein
Mkali, alisema Patrick alikatwa sehemu zake hizo na mpwa wake Zainabu
Said (32), baada ya kumkatalia kwenda kumfuata mumewe aliyekuwa kwa mke
mdogo.
Alisema tukio
hilo lilitokea juzi saa tisa usiku katika maeneo ya mashamba ya kijiji
hicho ambako walikuwa wakifanya shughuli za kilimo.
Alisema mume wa Zainabu ni Musa Said (40), aliyeenda kulala kwa mke mwingine ambaye jina lake halikupatikana na kumsababishia Patrick kukatwa sehemu zake za siri.
Alisema
baada ya kutokea kwa tukio hilo, ofisi ya kijiji imemkamata Zainabu na
kumpeleka polisi ambako ndiko maelezo zaidi ya kuhusiana na tukio hilo
yatatolewa huku Patrick akiwa amepelekwa Hospitali ya Tunduru.
yatatolewa huku Patrick akiwa amepelekwa Hospitali ya Tunduru.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msikhela, alisema atatoa ufafanuzi wa tukio hilo baada ya uchunguzi kukamilika.
