MKALI WA HIP HOP TANZANIA NAY WA MITEGO AZITETEA VIDEO ZISIZO NA MAADILI, CHEKI PICHA HIZI ZA VIDEO YAKE MPYA...NI SHEEEDAH...!!

Picha kadhaa zimevuja kwenye mitandao ya kijamii zikumuonyesha msanii huyo akiwa kimahaba na msichana kitandani zikimaanisha kuwa kuna video yake mpya inakuja.

‘’Yaah
hizo picha ni za video yangu mpya ambayo itatoka hivi karibuni na
kuhusu kwamba haina maadili mimi sijali na watu hajajua kama video za
namna hizo zinalipa kibiashara na lazima twende na wakati mbona video za
nje ambazo hazina maadili zinaonyeshwa hapa nyumbani? Alihoji Nay.

Akizungumzia kama BASATA wakiifungia video hiyo wakati ametumia gharama kubwa alisema kuwa hajali kwa lolote ila yeye yuko tayari kwa lolote.
Video hiyo ambayo itatoka hivi karibuni inaitwa ‘only one’