Jionee Huyu Aliyeamua kubadili sura na kufanana na Madonna




Watu wanawapenda mastaa, wapo wanaowapenda mpaka wanatamani wafanane nao, mara nyingi tumekutana na hizi story za watu ambao wamekuwa wakifanya majaribio ya kujibadilisha muonekano, maumbile yani ili tu afanane na staa wake anayempenda.

Jordan James alitumia dola 150,000 (zaidi ya mil 270/-) ili kujibadilisha afanane naKim Kardashian, safari hii ni Adam Guerra ambaye yeye jitihada zake alikuwa akizifanya ili afanane naMadonna.

Pesa aliyotumia ni paundi 75,000/- (sawa na mil. 210/-) na kutokana na ‘ukarabati’ ambao anataka kuendelea kuufanya kwenye mwili wake mpaka zoezi likamilike kiasi cha pesa kitakuwa kimefikia paundi 100,000/-Adamanasema anavutiwa sana na Madonna ndio maana anafanya kila kitu ili afanane naye.


“Nimewahi kupanda jukwaani nikamuiga Madonna..

nilipata mashabiki wengi, nimekuwa nikivutiwa naye kwa kila kitu, nimefanya maamuzi yangu binafsi kwa kutumia hela zangu ili nifanane naye kutokana na mapenzi yangu kwake, pia nimepanga kufanya ziara za kimataifa ili kuwadhihirishia watu jinsi gani navutiwa naye“-Guerra
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.