JAMAA ANUSA KIFO, WIZI WA FEDHA KWA MITANDAO YA SIMU
Kibano! Jamaa mmoja ambaye
jina halikupatikana mara moja, amejikuta akinusa kifo baada ya kula
kipigo ‘hevi’ wakati akifanya jaribio la wizi wa fedha kiasi cha
shilingi laki 450,000 kupitia huduma za fedha kwa mitandao ya simu.
Akiomba kuachiwa baada ya kupewa kichapo kikali.
Tukio
hilo lililoshuhudiwa na Ijumaa Wikienda lilijiri wikiendi iliyopita
maeneo ya Kijitonyama jijini Dar ambapo jamaa huyo alidaiwa kuingia
kwenye duka moja akijifanya anataka kutoa shilingi laki nne na nusu
(450,000/=) jambo lililomfanya wakala kumuonesha namba za kutolea kwa
uchangamfu akijua ni mteja wa kawaida.
Dakika
chache baadaye wakati wateja wengine wakiendelea kuhudumiwa, jamaa huyo
alionesha meseji kuwa ametoa kiasi hicho cha fedha kupitia moja ya
mitandao ya simu.
Wakala
huyo alipoichukua meseji ya jamaa huyo ili kuhakikisha muamala wake
alishangaa kuona meseji hiyo kuwa ni ya mtandao mwingine tofauti na
alioutaja huku ikionesha imeandikwa au kutumwa na namba ya kawaida ya
simu badala ya namba ya huduma hiyo ya mtandao husika.
Wakizidi kumshushia kichapo.
Wakala
huyo, Maulid Vedasto alishangaa na kuamua kumshikilia jamaa huyo
akimuitia mwizi ndipo wananchi wenye hasira kali walipofika na
kumzingira wakimtaka atoe maelezo ya kutosha ambapo njemba huyo ilikiri
kutaka kuiba jambo lililoamsha hasira za watu walioamua kumshushia
kipigo hevi nusura afe.
Akizungumza
na Ijumaa Wikienda, wakala huyo alisema kuwa jamaa huyo alifika mara ya
kwanza siku hiyo dukani kwake akitaka kutoa shilingi elfu sabini lakini
alighairi na kurudi baada ya muda mfupi akitaka kufanya jaribio hilo la
wizi.
Kichapo kikiendelea.
“Nilianza
kumtilia shaka mara ya kwanza alipokuja na kujifanya anataka kutoa
fedha huku akiwa na wasiwasi na kila mara alipokuwa akiwaona watu wengi
ndipo alipokuwa akiniongelesha akijifanya ana haraka ya kutoa fedha,
akiona watu wachache anasubiri,” alisema wakala huyo.Baada ya kunaswa
jamaa huyo alipekuliwa kwenye simu yake ambapo iligundulika kuwa kweli
meseji hiyo haikuwa ya mtandao husika huku akiwa hana salio.
Katika
kuhakikisha hilo, wakala huyo aliwapigia simu makao makuu ya mtandao
huo na kupata taarifa kuwa hakuna salio la aina hiyo lililohamishwa
kutoka kwenye simu ya jamaa huyo.Katika utetezi wake, jamaa huyo aliomba
watu wasimuue kwa kuwa ni tamaa za kidunia zilimponza huku akikiri
kufanya utapeli huo kwa kushirikiana na wenzake watatu ambapo
wamefanikiwa kutapeli mawakala kibao jijini Dar.