HATARI KWA MANCHESTER UNITED ....Van Persie apata jeraha..
Kilabu
ya Manchester United inasubiri kujua ubaya wa jeraha la mshambuliaji
wake Robin Van Persie baada ya mchezaji huyo kuondoka katika uwanja wa
Liberty akitumia magongo.
Van
Persie mwenye umri wa miaka 31 pia alionekana amefungwa mbamba katika
mguu wake wa kulia baada ya kupata jeraha katika mda wa lala salama wa
mechi dhidi ya Swansea ambapo Swansea waliibuka kidedea jumamosi.
Msimu
huu Robin Van Persie ameifungia Manchester United mabao 10,lakini
hakuweza kutolewa kwa kuwa United tayari ilikuwa imefanya mabadiliko
matatu.