AZAM WAPATA SARE TENA, TOFAUTI YA POINT NI 4 SASA



Mabingwa wa ligi kuu ya vodacom Azam fc wamepata sare ya 2 mfululizo na kupekea tofauti ya pointi baina yake na vinara wa ligi kuu yanga kuwa pointi 4.

Azam fc usiku wa leo wametoka sare ya bila kufungana na Tanzania Prinsons katika uwanja wa azam complex ikiwa ni kama mchezo wa oktoba 4 mwaka jana uliochezwa katika uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.

Katika mchezo wa leo kipa wa Prisons alifanya kazi ya ziada kuhakikisha azam fc hawapati goli lolote lile, kwa kuokoa hatari zote zilizokuwa zinaelekezwa kwake, katika mchezo ambao Prisons muda mrefu walikuwa nyuma wakizuia.

Kwa kipindi chote cha mchezo Prisons walikuwa katika eneo lao na kuwaacha azam fc wachezee mpira wanavyotaka, huku wakiwanyima mianya ya kutengeneza nafasi ya kupata goli.

Hii ni sare ya pili mfululizo toka waifunge El-merekh ya Sudan katika mchezo wa klabu bingwa Afrika, sare ya kwanza waliipata dhidi ya Ruvu shooting katika uwanja wa mabatini.

Kwa matokeo ya leo Azam fc wanabakia katika nafasi yao ya 2 wakiwa na point 27 wakati vinara yanga wakiwa na pointi 31 na kagera sugar wanaoshika nafasi ya 3 akiwa na pointi 24.
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.