UWOYA NA HEMEDI WAZICHAPA LIVE
IRENE UWOYA NA HEMEDI WATAKA KUZICHAPA LIVE LIVE BILA CHENGA
Picha hii ni ya wasanii Hemed na Jackline Uwoya ambapo ilidaiwa hapa Uwoya akiwa amekasirika baada ya Hemed kumsemea shiti wakirekodi filamu ya WAKE UP ya msanii Manaiki Sanga
Na Sabina Ramadhani
Filamu
mpya inayofananishwa na ile ya Expendables ya nje ya
nchi lakini sasa hii ya kitanzania imepewa jina la WAKE
UP wakati wa kuigizwa kwake ilikumbana na majanga makubwa
kufuatia mastaa wake kurumbana na hata kununiana huku
wakirekodi filamu hiyo ya msanii Manaiki Sanga.
Muongozaji
wa filamu hiyo Leah Richard Mwendamseke "Lamata" alisema
kuwa filamu hiyo ilikuwa na majanga makubwa sana hadi
kuja kumalikia kufuatia mastaa wengi kuleteana ubabe
wakati wakiigiza.
Lamata
aliendele kusema kuwa uigizaji wa filamu hiyo hadi
kukamilika umechukua miezi sita huku wakipambana majanga
makubwa" Kaka haikuwa rahisi kuwaweka mastaa wote hao
zaidi ya 30 pamoja kwa miezi sita ilikuwa shughuri sana
na ilipelekea wakati nilikuwa nafaunga na kusali ili
nimalize filamu ya watu" Alisema dada huyo
Hata
katika tukio la wazi ni lile ya msanii Hemed kutaka
kumpiga makosi ya kweli msanii Irene Uwoya wakati
wakiigiza sini yao na kupelekea kusimama kwa muda kupisha
ugomvi huo kwa wasingeweza kuendelea kurekodi wakati
hawako kwenye mudi nzuri,
Filamu
hiyo ambayo kwa sasa ipo hatua za mwisho kumalika huku
makampuni makubwa ya usambazaji yakipigana vikumbo
kupanda dau wasanii baadhi waliogiza ni Irene Uwoya,
Jackline Wolper, Gabo, Othuman Amri "King Majuto" Kajala,
Yusuph Mlela, Tausi, Aisha Boko, Hemed Suleiman,
Quickrocker, Kupa,Duma, Mama Abdul, Flora Mvungi, kwa
upande wa wanaumziki ni Country Boy, Nas B akiwemo
mwenyewe Manaiki Sanga ambae ndiye staa wa filamu hiyo.