Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Iramba Singida, Halima Mpitaamenusurika kifo baada ya kulipukiwa na kitu ambacho kinadhaniwa kuwa bomu la kutengenezwa kienyeji.
Kamanda wa Polisi Singida, Thobias Sidoyeka amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo nyumbani kwa Mkurugenzi huyo wakati akijiandaa
kwenda kazini, mlipuko huo ulitoka kwenye bahasha ambayo aliipokea juzi
kutoka kwa Katibu Muhtasi wake.
Ndani ya bahasha hiyo kulikuwa na ujumbe “Poleni sana, hatuwezi kufanya dili la milioni 90 halafu mkala peke yenu, sisi mkatudhulumu tukawaacha”, baada ya kuisoma alienda nayo nyumbani bila kujua kama kuna kitu kingine ndani.
Wakati
akijiandaa kwenda kazini siku ya jana ndipo mlipuko huo ulipotokea,
hakuna aliyekamatwa ila Polisi wanaendelea na upelelezi wakishirikiana
na JWTZ ili kubaini kama mlipuko huo ulitokana na bomu.