UMESKIA HII: SERIKALI YA PANGA KUPIGANA NA WACHAWI WOTE BONGO, JE? WATAWEZA SOMA MIPANGO YAO HAPA
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati meza) akizungumza
na waandishi wa habari kuhusiana na Serikali kuunda timu maalumu ya
kutembelea maeneo yaliyosugu kwa utekaji na mauaji ya albino nchini
ambapo timu hiyo inatarajiwa kuanza kazi wiki mbili zijazo kwa kuanza
na mikoa sugu ya matukio hayo ambayo ni Mwanza, Geita, Simiyu, Tabora
na Shinyanga na baadaye itafuata mikoa mingine. Kulia ni Mkuu wa Jeshi
la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu na kushoto ni Mwenyekiti wa Chama
cha Albino nchini (TAS), Ernest Kimaya. Mkutano huo ulifanyika katika
ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Picha na
Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.Picha na Emmanuel
Massaka
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
Serikali
imewapiga marufuku waganga wa jadi wanaotumia ramli kutokana na kuwa
chanzo cha mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino).
Hayo
yamesemwa leo na Waziri wa Mambo Ndani ,Mathias Chikawe wakati
alipokutana na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es
salaam,Chikawe amesema waganga wa jadi wanaotumia ramli wamekuwa
wakiwaambia watu kuwa kuua au kupata kiungo cha albino ni utajiri,kuwa
mvuvi wa mwenye mafanikio.
Chikawe
amesema Jeshi la Polisi na Chama Cha Wenye Ulemavu wa Ngozi (Albino)
wameunda timu maalum ya kufanya operesheni kwa waganga hao katika mikoa
mitatu ikiwa lengo ni kutokomeza mauji ya albino.
“Tunataka
kutokomeza mauaji ya Albino kwa timu hii ambayo tumeiunda itapita kila
sehemu na wale wote ambao watabainika watachukuliwa hatua na kesi hizo
zitapewa kipaumbele na Mwendesha Mashitaka Nchini (DPP)”alisema Chikawe.
Operesheni
hiyo ya kutokomeza mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino)
itafanyika katika Mikoa mitano ambayo inaonekana ni sugu katika matukio
hayo, nayo ni Mwanza,Tabora,Simiyu,Shinyanga pamoja na Geita.
Aidha
alisema kuhusu serikali kutoamini ushirikina wa kazi hiyo pia itafanywa
pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala Mikoa na Tawala za Mitaa
(Tamisemi) ambapo sheria ya kuwabana itakapopatikana.

