TUJIKUMBUSHE UFISADI MKUBWA ULIOWAHI KUFANYWA NCHINI NA KUIGHARIMU NCHI
MUNGU ni mwema na ndiyo maana leo wasomaji wa safu hii mnaisoma huku mkiwa na afya njema. Tumhimidi Mungu aliyetuumba milele, amina.
Baada ya kusema hayo niseme machache kuhusu mikataba mibovu ambayo imeiingizia taifa hili hasara kubwa ambayo taifa linahujumiwa.
Baada ya kusema hayo niseme machache kuhusu mikataba mibovu ambayo imeiingizia taifa hili hasara kubwa ambayo taifa linahujumiwa.
Mikataba
hii inanifanya nijiulize, baadhi ya watu, Watanzania wanasoma na kupewa
nyadhifa za kufanya kazi kwa niaba ya nchi walisoma ili kuiangamiza
nchi au kuitetea isizame?
Kati ya mwaka 1995 na 2007, nchi yetu ilighubikwa na mikataba ya uwekezaji ya kifedhuli, iliyosababisha mabilioni ya fedha kukwapuliwa na mafisadi wa ndani na nje ya nchi na kufichwa katika mabenki ya ughaibuni.

Baadhi
ya mikataba hiyo hatari ya uwekezaji, ni pamoja na ule wa mradi wa
Independent Power Tanzania Ltd (IPTL) na serikali, kupitia Shirika la
Ugavi wa Umeme nchini (Tanesco).
Chini
ya mkataba huo wa miaka 20, nchi imeporwa mabilioni ya fedha na
inaendelea kuchunwa na kutupwa gizani kwa kukosa umeme, ingawa
itaendelea kuilipa IPTL zaidi ya shilingi bilioni 5.0 kwa mwezi kwa
umeme usiokuwepo, kuanzia mwaka 1999 hadi 2019.
Walioiingiza
nchi katika kashfa hiyo wanafahamika kwa majina, lakini wamekumbatiwa
na kutakaswa ili watakasike na baadhi ya watu wasiokuwa na uchungu wa
nchi hii wanawaona ni wajanja!
Kashfa nyingine zenye kuhusisha mabilioni ya fedha, ni pamoja na ile ya EPA (ilihusisha shilingi bilioni 133), ununuzi wa rada na ndege mbovu ya rais kwa kile kilichoelezwa na Waziri wa Fedha wa wakati huo, Basil Mramba kwamba rais hawezi kupanda punda kama Yesu wa Nazareth. Ndege hiyo mbovu ilinunuliwa shilingi bilioni 40.

Nyingine
ni ubinafsishaji wa Benki ya NBC na uuzaji wa nyumba za serikali kwa
bei ya kutupa, pamoja na kuuzwa kwa Mgodi wa Makaa ya Mawe Kiwira, bila
kusahau sakata la mradi wa umeme wa kitapeli wa Richmond/Dowans;
Loliondo, ufujaji wa shilingi bilioni 150 za Mfuko wa Uagizaji Bidhaa
Nje (CIS) na mikataba mibovu ya madini, kwa kutaja michache tu.
Haya yametokea na hakika wasomi wote waliohusika na hujuma hii wanapaswa kulaaniwa na wananchi wote wazalendo wa nchi hii.
Serikali
imejitahidi kuficha ukweli wa kashfa hizi lakini Mungu amewapenda zaidi
wananchi na haya mambo yakajulikana. Kashfa moja kabambe, inayohusu
Mradi wa Mgodi wa Meremeta ililipuliwa bungeni na ilifikia Bunge
kuitaka serikali iwasilishe hesabu za kampuni hiyo kwa Mkaguzi na
Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG) ziweze kukaguliwa ili kukata mzizi wa
fitina.
Tunaipa umuhimu
wa pekee kashfa hii ya Meremeta kwa sababu ni kielelezo cha wazi kwa
serikali kuhusishwa moja kwa moja katika uporaji wa rasilimali za taifa
na kugeuka mbogo kuwahadaa wananchi baada ya kugunduliwa kwa kisingizio
cha fedha zilizoporwa kutumikia usalama wa nchi.X
Katika
kashfa hiyo, zaidi ya shilingi bilioni 155 zililipwa kutoka Benki Kuu
(BoT) kwenda Benki ya NedBank ya Afrika Kusini kama malipo ya mkopo
uliodhaminiwa na serikali kwa mradi huo wa uchimbaji dhahabu.
Serikali ilibanwa na Bunge na kuagiza mahesabu yakaguliwe, haikutii na aliyekuwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ( CAG) Ludovick Utouh, alinukuliwa baadaye akilalama: “Nitakagua nini wakati sijapata hesabu zenyewe kutoka serikalini…?

Kampuni ya Meremeta, ambayo baada ya mambo kufichuka ilibadilishwa jina kiujanjaujanja na kuitwa Tangold.
Wabunge
walikatazwa kuijadili kwa sababu za kiusalama. Je, kuna ukweli gani
kwamba Kampuni ya Meremeta haizungumziki kwa sababu inagusa Usalama wa
Taifa? Je; ni kampuni ya serikali? Malipo hayo na mengine ndiyo
yaliyozua utata na Bunge kuagiza hesabu zikaguliwe.
Napenda
kutaja wazi hapa kwamba Serikali ya Awamu ya Nne ya Rais Jakaya Mrisho
Kikwete, kwa namna yoyote ile, haihusiki na sakata zote hizi, ingawa
inazijua fika, hivyo, imejitahidi kuziatamia bila mafanikio kwa njia ya
kufunika kombe mwanaharamu apite na mambo kama hayo yamemgharimu
aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredirick Werema.
Serikali
ifahamu kwamba kwa misingi ya sheria, kitendo cha mtu kufunika kosa
lililotendwa na mtu mwingine, kwa lengo la kumwepusha sheria isichukue
mkondo wake, kinamfanya mtu huyo mwenye kutaka kumwokoa mwingine kuwa
mshiriki wa kosa hilo kwa kiwango sawa na cha mtuhumiwa halisi wa kosa.
Kwa hiyo, viongozi wanaowalinda au kuwasafisha mafisadi wana hatia ya ufisadi uleule wa wale wanaowaokoa.
Nia
ya kukumbushana ufisadi huu ni kuwataka wanaokabidhiwa dhamana ya
kulinda rasilimali za nchi hii kuwa na uzalendo wa kweli na kuachana na
rushwa au hujuma kwa taifa.
Jipu limepasuka, siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.