MTANGAZAJI AVUNA MIL.28
MTANGAZAJI wa
runinga Maimartha Jesse, ameweka wazi kuwa pamoja na watu kulalamika
kuwa mwaka uliopita ulikuwa mgumu kifedha kwa upande wake amefanikisha
kuingiza kiasi cha shilingi milioni 28 ambazo amezipata kupitia kazi
zake za kila siku ikiwemo ya kundi lake maarufu la Baikoko.
Maimartha
alifunguka mchongo huo wa kudaka kiasi hicho cha pesa baada ya
kuzungumza na mwandishi wetu, ambapo alisema kuwa huwa anafanya kazi
zake si kwa kumtazama mtu usoni na hiyo ndiyo sababu kubwa iliyomfanya
kuvuna kiasi hicho cha pesa.
“Nimepata
pesa nyingi maana kama ningekaa tu nyumbani nisingeweza kupata hata
hizo milioni 28, namshukuru Mungu kwa sababu nimeweza kufanya kazi zangu
kwa ubora na kupata kiasi hicho, lakini kifupi ni kwamba sijafanya dili
feki za kupata pesa,” alisema Maimartha.