SHULE YAGEUZWA DANGURO ONA PICHA HAPA HATAREEEEEEEEE
Danguro hatari linaloendesha shughuli zake katika eneo la shule limefichuliwa baada ya kumnasa mwanamke aliyedai ni mke wa mtu akifanya uzinzi na mtu ambaye hakufahamika mara moja.
Tukio hilo la aibu lilijiri ndani ya eneo la shule ya msingi Shekilango, iliyopo Mapambano, Sinza jijini Dar es salaam, hivi karibuni ambapo mke huyo wa mtu alikuwa akichepuka.
Wawili hao, baada ya kukamatwa wakifanya ngono hadharani walitiwa kizuizini kabla ya vijana wanaodaiwa kuchukua posho kwa wanaofanyia mambo yao kwenye danguro hilo kuanzisha vurumai ingawa walidhibitiwa huku jamaa aliyekuwa anahudumiwa akitoka nduki.
Akizungumza na mwandishi, mwanamke huyo aliomba asamehewe na kusema kwamba kinachomsababishia kufanya shughuli hiyo ni ugumu wa maisha na kundi la watoto anaowalea ambao baba yao hana ajira.
Baada ya mwandishi kutaka kuzungumza na mumewe ili kujua kama anafahamu kuwa mkewe anafanya biashara haramu ya kuuza mwili, mwanamke huyo alidai kwamba mumewe hana simu.
"Ni aibu, asubuhi watoto wanafagia kondom, tunakosa cha kuwaambia, hii ni hatari kwa kweli na tunaomba mamlaka zinazohusika zilifanyie kazi jambo hili," alisema mwalimu Kilavo Charles wa shule hiyo baada ya kuzungumza na mwandishi kuhusiana na sakata hilo.