MAMBO 10 MUHIMU YA KUKUMBUKA KATIKA SOKA LA UINGEREZA MWAKA 2014

Kuna mambo lukuki ya kustaajabisha na kufurahisha katika mwaka huu unaomalizika hususani kunako soka la Uingereza na hata wakati mwingine inaweza kuwa vigumu kubaini yalovutia zadi.  Mfano, ni namna ambavyo Sunderland na Crystal Palace walivyopambana na hatimaye kujinusuru na panga la kushuka daraja; namna ambavyo Manchester City waliweza kuipokonya ‘tonge’ Liverpool na kushinda taji la ligi kuu mara ya pili ndani ya miaka mitatu au namna ambavyo mipango ya kurithi viatu vya mkongwe Sir Alex Ferguson ilivyokwenda, kiwango cha Mchile Alexis Sanchez na mengine mengi.
Hata hivyo, pamoja na ugumu huo makala hii inakuletea mambo kumi ambayo mwandishi anaamini ni ya kukumbukwa zaidi maana kuna wakati kuwa shabiki wa klabu za ligi hii yenye ushindani wa hali ya juu na umaarufu unajikuta mwenye kuambulia machungu zaidi kuliko furaha.
  1. Nyuso za Aibu
Ilikua ni katika michuano ya Kombe la ligi (Capital One) na msimu huu ikuwa ndo kwanza ungali katika wiki mbili za awali ambapo klabu yenye historia kubwa nchini Uingereza ya  Manchester United ilianza na kikosi cha nyota wake wachanga isipokuwa kwa Shinji Kagawa, Danny Welbeck na Javier Hernandez (ambao walioneshwa mlango wa kutokea baadae). Kilichoacha kumbukumbu si kuachwa kwa wachezaji hao bali kichapo cha ‘mbwa mwizi’ cha bao 4-0 toka moja ya klabu ya madaraja ya chini ya MK Don mnamo Aug. 26

  1. Jeuri
Hii inamhusu bosi wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho ambaye mara kwa mara amejikuta katika mgogoro na makocha wa timu pinzani sababu ya kauli zake tata na za kichokozi. Mfano ni namna alivyojidai kushindwa kutamka kwa usahihi jina la bosi wa City, Manuel Pellegrini au namna alivyomwita Arsene Wenger  “bingwa wa kufeli”.

Kuna wakati pia ambapo bosi huyo alinukuliwa kutoa matamshi ya kutowaheshimu Roy Keane na staili ya nywele ya meneja wa zamani wa Aston Villa, Paul Lambert. Hii ilikuwa mnamo Septemba 27 ambapo muda wa mchezo ukiwa haujaisha huku timu yake ikiwa mbele kwa mabao 3-0 uwanjani Stamford Bridge Mourinho aliamua kuondoka uwanjani lakini kabla ya hapo alikuwa mwenye kuwaaga meneja Lambert, na msaidizi wake Keane.
  1. Mwana Mpotevu
Kwa washabiki wa Arsenal haikuwa kumbuku njema sana japo walifanikiwa kutwaa taji la FA baada ya kusubiri vikombe kwa muda mrefu.
Hii si kumbukumbu njema kwao kwani inamhusisha nyota Fabregas ambaye mpka sasa ametoa pasi 13 za mabao kunako ligi kuu msimu wa 2014-15.

Kilichoshangaza ni namna Cesc fabregas alivyoitosa Arsenal na kujiunga na Chelsea ilihali mapema majira ya kiangazi alipata kunukuliwa akisema “Arsenal iko moyoni mwakena daima itabaki
Ikumbukwe ni Bosi wa washika bunduki, Arsene Wenger ndiye aliyemtoa toka shule ya soka ya klabu ya Barcelona, La Masia akiwa na umri wa miaka 16 na kumfanya mchezaji kinda zaidi katika kikosi cha Arsenal na hata alipoanza harakati zake za kutaka kurudi alikokulia aliahidiwa na meneja huyo kuwa kama atacheza kwa msimu mmoja zaidi angeruhusiwa. Cesc ni kama mwana mpotevu kwani hakufanikiwa kurithi nafasi ya Xavi kama alivyotaraji na badala yake akajikuta akirejea katika ligi iliyompa mbinu lukuki ingawa amechagua jezi za Bluu na si Nyekundu
Mbaya zaidi ghafla tu zilibuka taarifa za si Fabregas aliyeikataa Arsenal bali Arsenal ndiyo ilomkataa Fabregas.  Inasemekana bosi Wenger hakuona namna ambavyo cesc angepata nafasi mbele ya utitiri wa viungo wake wachezeshaji kama Mesut Ozil, Santi Cazorla, Jack Wilshere na Aaron Ramsey. Ikiwa ni miezi mitano (5) baadaye nyota huyo ameisaidia Chelsea kukaa kileleni huku akitishia kufikia rekodi ya nyota mfaransa Thierry Henry ya pasi za mwisho 20 kwa msimu.
  1. Mchawi
Tofauti na kumtizama Golikipa akiokoa michomo ya hatari kwenye luninga ni maajabu zaidi pindi unapoweza kushuhudia mambo hayo yakifanyika kwa macho yako. Hii inamhusu mlinda lango wa manchetser united David de Gea ambaye umahiri wake katika kipindi cha pili kwenye pambano dhidi ya mahasimu wao liverpool itaendelea kukumbukwa na kukumbukwa. Akiwa ndio kwanza na umri wa miaka 24, De Gea alikuwa kama mchawi pale alipomudu kuokoa kwa ustadi mkubwa mipira iliyoonekana kama mabao ya wazi toka kwa wachezaji wa Liver Raheem Sterling na Mario Balotelli. Mashambulizi hayo ya ana kwa ana yaliwaacha hata nyota wengi wa Liver katika mshiyuko mkubwa.

Wakati umati ukijua ni goli kunako hali ambayo Sterling angefunga mara 2, na Balotelli mara 3 wote walijikuta wakiambulia patupu na kujikuta wakiishia kutikisa vichwa vyao wasiamini kwa kilichotokea. Mfano katika hali ya kushamgaza shuti kali lake mario ambalo ni wazi lilikua zaidi ya uwezo wa mwanadam wa kawaida hatua sita tu kutoka lilipo lango la United huku mlinda lango De Gea, akiwa anatizama upande mwingine wa lango (marikiti) aliweza kuuchezesha mwili wake kwa ustadi mkubwa na kuugusa mpira kwa mkono wake ukaishia kugonga nguzo ya goli.
Kufuatia maajabu hayo De Gea, amejikuta akisifiwa na kupachikwa sifa kibao na washabiki wa United baadhi yao wakiwa waliohoji uwezo wa kipa huyo mwaka mmoja ulopita ambapo aliendelea kuaminiwa na babu Ferguson kwa sasa wanashereka kumpata mlinda lango mlirthi sahihi wa Peter Schmeichel na Edwin van der Sar. Kwa mujibu wa wachambuzi mbaimbali kunako dakika hizo 45 za kipindi cha pili alikuwa bora kuliko hao magwiji walotajwa.
  1. “Ndonga” ya hatari
Unaikumbuka ndonga ya Zinedine Zidane kombe la dunia 2006!?. Basi mnamo machi moja huku Newcastle ikiongoza bao 3-1 dhidi ya Hull City, meneja mwenye miaka 53 alifanya tukio la kushangaza kwa mchezaji wa timu pinzani kiasi cha kuzua maswali watoto wanajifunza nini
Wakubwa hupigana na wakubwa wenzao na si watoto ila pasipo kujali hilo meneja wa Newcastle Alan Pardew alimtwanga kiungo wa Hull City David Meyler punde aliposukumwa ili kupisha njia na mchezaji huyo kuchukua mpira ulokua umetoka nje.

Na kwa kuwa tukio lilimhusisha meneja basi hata baadhi ya washabiki wa kutupwa wa klabu hiyo waliona ndio ulikuwa wakati sahihi wa kumshutumu bosi huyo ili aondolewe klabuni hapo. Hata hivyo, klabu hyo badala ya kumfukuza iliishia kumpa onyo la maandishi na faini ya $160,000
  1. Jeshi la Mtu Mmoja
Kuna mambo machache sana yanahesabika katika maisha mfano jua litachomoza asubuhi, jua litatuama wakati wa machweo. Ndivyo nyota Sergio Aguero alivyoisambaratisha Spurs.

Inawezekana nyota huyo wa man city akawadhihirisha jinsi gani alivyo hatari kwa namna alivyoweza kufunga bao 33 katika michezo 47 ya ngazi ya klabu na taifa kwa mwaka 2014 lakini kwa namna alivyoisambaratisha Spurs ni wazi alihitimisha dhana ya kwamba kukosekana kwa Luis Suarez kunamfanya abaki mchezaji bora zaidi katika ligi hiyo.
Mnamo Novemba 25 mwaka huu achilia mbali suala la Bayern Munichen kuwa pungufu aliweeza kufunga bao tatu pekee katika michuano ya klabu bingwa ulaya na hivyo kudhihirisha kwanini anastahili kuwekwa katika kundi la wamaliziaji mahiri. Hata nyota kama Lionel Messi na Cristiano Ronaldo ni wazi walivutiwa na uwezo wa nyota huyo ikizingatiwa ilikuwa nafasi tatu bao tatu teena dhidi ya miamba ya Bayern.
Na pengine kama siyo majeruhi ya mara kwa mara katika mwaka huu yaliyomkosesha michezo kadhaa pamoja na kushiriki kombe la dunia akiwa hayupo sawa asilimia mia, Agueroa ambaye anaaminika kuwa na uwezo mahiri wa kuvizia sawa na gwiji toka Brazil, Romaria ambaye kiumbile ni kama wanaendana angeefanya makubwa zaidi. Na bado  inaaminika hata Romario hakuwa mahiri sana wa kunyumbulika na kuwatoroka walinzi kama  Aguero
Sawa kuhusu bayern, mfano anuai ni namna alivyoiadhibu Spurs mara nne peke yake uwanjani Etihad hapo october 18, katika ushindi wa bao 4-1. Hii imemfanya Aguero kuifunga spurs mara 9 katika michezo 6 na kama siyo kukosa peenati katika pambano hilo pengine hali ingekua mbaya zaidi kwa spurs.
Na inaaminika kama City watafanikiwa kumfanya nyota wao huyo asiwe majeruhi ni wazi wataendelea kutwaa vikombe na vikombe, sema kuumia umia kwakee mara kwa mara ndio kunatia wasiwasi.

  1. Goli za ajabu
Gwiji toka Brazil Pele katika maisha yake ya soka ameacha alama na pengine kuondoa ubishi kunako uwzo wa kufumania nyavu lakini kumbukumbu za mwaka huu zinatuonesha nyota kama Jonjo Shelvey pia wanaweza alama hizo.
Kiungo huyo wa klabu ya Swansea alifunga bao murua akiwa katikati ya uwanja bao ambalo hata nyota bora zaidi katika ulimwengu wa soka hakuwahi.

Pele amewahi kujaribu pasipo mafanikia katika pambano la kihistoria dhidi ya Czechoslovakia  mwaka 1970 lakini haikua tabu kwa Shelvey ambae aliweza kuupiga mpira karibu na katikati ya uwanja na kumpita mlinda lango wa Aston Villa Brad Guzan.
Hata hivyo hakuwa Shelvey peke yake kwani hata naodha wa Manchester uniteed, Rooney aliushangaza ulimwengu katika pambano dhidi ya West Ham mapema tarehe 24 mwezi machi.
Hakika ni ajabu kwa ligi ya uingereza kushuhudia takribani mara 2 magolikipa wakichupa pasipo mafanikio na kufungwa goli za takribani umbali wa mita 50. Ili kufunga unahitaji mbinu sahihi, nguvu, na shuti za hali ya juu huku golikipa wa timu pinzani akiwa hayuko langoni.
  1. Kuteleza
Wakati wengi wakiamini Liverpool ingeweza kurudia maajau kama yale ya Instabul, Uturuki, hasa mashabiki wa Liverpool naodha na mkongwe wa klabu hiyo Steven Gerrard aliteleza na hivyo kutoa mwanya wa kuadhibiwa na Chelsea uwanja wa nyumbani, Anfield.

Hii ilihitimisha ndoto yao ya kulitwaa taji walilolikosa kwa mda mrefu (miaka 24). Ikumbukwe tukio hilo lilitokea ikiwa zimepita takribani wiki mbili toka Liverpool iiifunge Manchester City katika mchezo ambao ulitabiriwa kama mechi ambayo ingeamua bingwa wa ligi hiyo na kisha naodha huyo mwenye heshima kuwakusanya na kuwambia wenzake si muda wa kufanya makosa.
Ghafla, kwa mshangao wa wengi ni yeye ndiye aliyefanya kosa kufuatia kushindwa kuumudu mpira alorudushiwa na mlinzi, Mamadou Sakho na hatimaye kutoa nafasi kwa mshambuliaji Demba Ba kuwaadhibu.
  1. Chizi mwenye Kipaji
Ni wazi ligi kuu ya Uingereza inammisi Luis Suarez. Hii inatokana na uwezo wake maridadi kila alipopata mpira na kukimbia nao, namna alivyowanyanyasa mabeki na kuwafanya kuwa na nyuso za wasiwasi sambamba na mabao yake murua ya mara kwa mara
Kwa uwezo alokua nao ni wazi alikua na kipaji cha pekee chenye kuvutia kutazama sio tu kwa wanaliverpool bali yeyote mwenye kupenda kutizama wachezaji wenye viwango vya dunia. Nyota huyu toka Uruguay alikuwa mahiri katika hilo Suarez’s genius still couldn’t win Liverpool a league title.

Na pamoja na kuwa hawakuweza kushinda taji la ligi kuu ilihali alionesha kipaji chake matata bado mwaka 2014 unabakiza kumbukumbu juu yake. Na hata mara baada ya sare dhidi ya Crystal palace Selhurst Park ambayo ilififisha ndoto zao za kutwaa ubingwa mbele ya Manchester City nyota huyo alilia sana mara baadyua ya pamabano husika pngine sababu alijua ni moja ya michezo yake ya mwisho katika jezi za klabu hiyo au machungu ya kupoteza alichokipigania kwa mda mrefu
Na hata alipoondoka ikiwa ni takribani miezi mitano sasa klabu yake hiyo bado iko taabani ingawa ndio kwanza mzunguko wa kwanza umemalizika.
  1. Taji
Baada ya kuhangaika kwa miaka tisa pasipo kutwaa taji lolote hatimaye iliwekwa kumbukumbu kunako historia ya klabu hiyo pale walipoifunga Hull City 3-2 na kunyakua taji la Kombe la FA.
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.