MWILI WA MTU ALIYEGOGWA NA TRENI HUKO MOROGORO WAGAWANYIKA VIPANDE VIPANDE
Mtu
mmoja ambaye hakuweza kufamika mara moja amegongwa na TRENI katika
eneo la kingolwira nje kidogo ya mji wa morogoro na viungo vya mwili
kusambaa zaidi ya mita mia moja.
Paparazi
imeshuhudia askari na wananchi wakiokota vipande vya viungo vya mwili
ikiwemo miguu na mikono na hawakufanikiwa kukipata kichwa ingawa
viungo vingine kama miguu mikono kifua vilipatikana ambapo wananchi
wa eneo la kingolwira wamesema huenda mtu huyo alikua mlevi alikua
anavuka reli usiku bila kuchukua tahadhari …muhamed juma ,shuhuda .
Station
master mkoa wa morogoro Flavian Nyawale amesema wamekabidhi
jeshi la polisi tukio hilo ili kufanya uchunguzi na kutoa tahadhari
kwa wananchi watembea kwa miguu kuach akutembea kando kando ya reli na
kuchukua tahadhari wakati w akuvuka katika makutano ya reli na
barabara ili kuepusha matukio ya ajali zisizo za lazima.
Kamanda
wa reli Enginea Simon Chillery akizungumza kwa njia ya simu akiwa
njiani kuelekea nachingwea amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na
amesema mtu huyo ambaye hakufahamika jina lake anakadiriwa kuwa na umri
kati ya miaka 35 na 40 na uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na
kuwakumbusha wananchi kuheshimu sheria za reli kama ilivyo sheria za
barabarani kwa watembea kwa miguu na wanaendesha vyombo vya moto
wanapovuka reli.