MCHUNGAJI MTIKILA AMSHITAKI ASKOFU MOKIWA KWA KUMSHIKA MAKALIO HADHARANI.! KESI SASA YA PAMBA MOTO
Mchungaji
Christopher Mtikila amefungua kesi katika mahakama ya hakimu mkazi
Kisutu kumshitaki Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglican Tanzania Dk.
Valentino Mokiwa.
Msingi
wa kesi ni kwamba Askofu Mokiwa alimshika makalio Mtikila na kwamba
kitendo hicho kilichotokea Juni 25 mwaka jana walipokutana maeneo ya
Ilala, kimemdhalilisha.
Mtikila
alikuwa ameitwa na Askofu kujadili tamko la la Mtikila kwamba Kanisa
la Anglican linajihusisha na ufisadi, ukiwemo wizi wa vifaa vya
Hospitali ya Mission ya Millo iliyoko Ludewa mkoani Njombe.
SOMA HAPA
HIVI KWANINI FACEBOOK IMEKUWA UWANJA WA KUJINADI NA KUJIUZA KWA WADADA WENGI WA HAPA BONGO..
Mtikila
alivyoitwa na Askofu Mokiwa ili kujadili hilo alifika na wenzake
watatu wa taasisi ya Liberty International Foundation na wakakaribishwa
kwenye moja ya jengo la dayosisi ya St. Nicholous, usiku wa saa 03:00.
Muda
mfupi baada ya kikao kuanza, Askofu Mokiwa ambaye alikuwa na wenzake
saba, alisimama na kuwataka wajumbe wote wakaguliwe kama kuna mtu ana
kinasa sauti. Baadae Askofu Mokiwa nae alisimama na kuungana na wenzie
kuwakagua kina Mtikila baada ya kuhakikisha mlango umefungwa.
Katika
upekuzi huo ndipo tuhuma hizo zilipopatikana kutokana na madai kwamba
operesheni hiyo ilienda mbali zaidi ya lengo la kawaida.
Wakili
wa Upande wa mashtska aliiambia mahakama kuwa, "Mlalamikiwa alitangaza
kuwa, kila mtu aliyekuwemo kwenye mkutano lazima apekuliwe na kwamba
atakayekataa angetumia nguvu, kwa kuwa alikuwa na bastola, hakuna
aliyebisha."
Alisema
kisha akaendelea "Mshtakiwa (Mokiwa) alianza kupenyeza mikono yake
kwenye shingo kuelekea chini kisha huko chini mikono ya mlalamikiwa
ilionekana waziwazi ikipapasa makalio ya mlalamikaji".
Mchungaji Mtikila ameiomba Mahakama imwamuru Askofu Mokiwa alipe fidia ya shs. bilioni moja kwa kumdhalilisha.
Madhara
zaidi ya kitendo hicho ni pamoja na mfadhaiko, masikitiko, wasiwasi,
aibu katika jamii na kupata shinikizao la damu la mara kwa mara na
matatizo ya moyo kila anapokumbuka kitendo hicho.
Kesi inasikilizwa kwenye Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, chini ya Hakimu Agness Mchome.
