MAAFA YA MVUA HUKO MOROGORO NI ZAIDI YA ILE YA DAR WAKAZI WAKOSA SEHEMU ZA KUSHI
MVUA KUBWA ZILIZONYESHA ZASABAISHA MAFURIKO MJINI MOROGORO...SOKO KUU LAZINGIRWA NA MAJI
Soko
Kuu la Morogoro likiwa limezingirwa na maji jana baada
ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha mafuriko katikati
ya mji kutokana na mto Kikundi kujaa mchanga.Mvua
kubwa zilizonyesha kwa muda mfupi mjini Morogoro
zimesababisha mafuriko baadhi ya barabara kushindwa
kupitika na maji kujaa katika baadhi ya maduka. Wakazi
wa mji wa Morogoro wakizungumzia mafuriko hayo
wamelalamikia miundombinu mibovu ya barabara kutokana na
kuziba kwa mitaro ambapo wameitaka halmasauri ya mji wa
Morogoro kuzibua mitaro hiyo huku baadhi ya
wafanyabiashara wakilalamikia kupata hasara
Katika
mto kikundi uliopo mjini Morogoro umepoteza uelekeo na
kumwaga maji katika soko kuu la mji wa Morogoro na
kusababisha maji kujaa katika maduka huku baadhi ya
magari yakiingia kwenye mitaro na baadhi ya bodaboda
zikiwa na abiria zime zama katika majina kulazimika
kuvutwa.
Kaimu
mkurugenzi wa manispaa ya Morogoro Phelemon Magesa
akizungumzia alalamiko hayo ya wananchi hao amesema
manispaa wanajitahidi kufanya usafi lakini tatizo liko
kwa wananchi wemyewe kutupa taka kwenye mitaro na
kusabisha mitaro hiyo kuziba na maji kupoteza ueleko na
kujaa katika makazi ya wananchi