LULU ATOA SIRI YA MAFANIKIO YA MASTAA WA KIKE BONGO

ELIZABERTH
Michael‘ Lulu’ amefunguka kuwa wasanii wa kike wa filamu wana biashara
nyingine iliyojificha ndani ya ile ya filamu ambayo inawalipa zaidi.
Lulu
amepasua kuwa wasanii hao wanawategemea mapedejee kuendesha maisha yao
huku wengi wakiamini kwamba mabinti hao wa Bongo Movie wanalipwa vizuri
kutokana na filamu wanazoigiza.
“Ukweli
hauko hivyo, hali hii inatokana na wengi wetu kudumaa na hatuwazi
kufanya mambo makubwa kwa kuigiza na wasanii wakubwa lakini hakuna
anayeliona hili,” alifafanua.
“Hakuna
anayefirikiria kuigiza na wasanii wa kimataifa kama Ritha Dominic ili
sanaa imlipe na wengi wanawategemee mapedejee au biashara zisizo rasmi,
kwani filamu inaonekana ipo juu lakini wahusika wake wanalipwa kwa
staili nyingine kabisa,” alisema.
Mwanaspoti