CMM SASA YA GAWANYIKA KATIKA MAKUNDI
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) na Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Mohammed Gharib Bilal, Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai (kulia) na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, wakiimba nyimbo ya chama hicho kabla ya kuanza kwa kikao cha kamati maalum ya chama hicho kilichifanyiaka jana katika ofisi kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar. Picha na OMR
Dar es Salaam.
Habari kuwa Kamati Kuu ya CCM inayokutana Zanzibar kesho itajadili
hatima ya vigogo sita wa chama hicho waliopewa onyo kwa kuanza kampeni
za urais mapema, zimezidi kuyaweka makundi ya vigogo hao njiapanda.
Pamoja
na ajenda nyingine, jambo kubwa linalozisumbua kambi hizo ambalo
lilizifanya zipige simu jana chumba cha habari cha gazeti hili, ni
kutaka kujua ni suala gani litajadiliwa, wagombea gani watajadiliwa na
uwezekano wa ama kufutiwa onyo lililotolewa Februari mwaka jana au
kuongezewa adhabu.
Hata hivyo, taarifa kutoka ndani ya kikao
cha Sekretarieti ya chama hicho iliyokutana juzi Dar es Salaam, ilisema
suala hilo halitakuwa moja ya ajenda za mkutano huo wa kesho, licha ya
Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana kueleza akiwa Tanga kuwa moja ya
ajenda itakuwa suala la maadili.
Miongoni mwa ajenda
zinazotajwa ni ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliomalizika mwishoni
mwa mwaka jana, kalenda ya chama kwa mwaka huu na sherehe za miaka 38
ya CCM zinazotarajiwa kufanyika Songea mkoani Ruvuma.
Vyanzo
vingine vya habari vimeeleza kuwapo pia kwa ajenda ya hali ya siasa
inayohusishwa na harakati za urais, hususan kwa vigogo wanaopishana
kusaka nafasi hiyo na wale waliotajwa katika kashfa ya Akaunti ya Tegeta
Escrow.
Kamati Kuu inatarajia kutumia vikao hivyo kuangalia
namna ya kupata wagombea watakaokubalika kwa wananchi kuelekea kwenye
kinyang’anyiro cha urais, wabunge na madiwani.
Akiwa katika
ziara ya kuwashukuru wananchi kwa kuipa CCM ushindi kwenye Uchaguzi wa
Serikali za Mitaa mkoani Tanga, Kinana alisema chama hicho kitafanya
kikao hicho kwa lengo pia la kupitia masuala mbalimbali yanayokihusu.
Alisema
salamu za CCM kwa Watanzania kwa mwaka huu ni ahadi ya kuweka mkazo
katika maadili kwa viongozi wake na itafanya tathimini kwa lengo la
kujipanga kwa Uchaguzi Mkuu.
Alipoulizwa kuhusu ajenda katika
vikao hivyo wiki iliyopita, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape
Nnauye alikuja juu na kusema hakuna kitu kama hicho. “Hata mkiiandika
vibaya CCM itashinda tu,” alisema hivi karibuni.
Vigogo
waliopewa onyo na CCM ni pamoja na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi
na Teknolojia, January Makamba na mawaziri wakuu wa zamani, Edward
Lowassa na Frederick Sumaye.
Wengine ni Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Steven Wasira na aliyewahi kuwa Waziri
wa Nishati na Madini ambaye ni Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja na
waziri waliokumbwa na kashfa ya escrow ni Profesa Anna Tibaijuka na
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhong-