BANDARI KUFURU TUPU UFISADI WAKE NI ZAIDI YA ULE WA ESCROW

Wakati Msajili wa Hazina amebariki posho mpya za safari za ndani kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA) kuwa Sh 500,000 kwa siku kuanzia Januari 2, mwaka huu, imebainika kuwa walishaanza kulipana hivyo tangu mwaka 2011.
Hayo yalibainika wakati wa Kamati ya Bunge Hesabu za Serikari (PAC), ilipokutana na Menejimenti ya TPA jijini Dar es Salaam.
Kutokana
na kamati hiyo kubaini posho hizo, zilianza kutumika hata kabla ya
kupitishwa, imeiagiza Menejimenti ya TPA kuhakikisha wafanyakazi wote
waliolipwa viwango vipya vya malipo ya safari kabla ya kuruhusiwa na
Msajili wa Hazina wanazirejesha.
Agizo
hilo la kurejeshwa kwa fedha za posho, limetolewa na Mwenyekiti wa PAC,
Zitto Kabwe, aliyesisitiza kuwa ni makosa kwa taasisi kuanza kutumia
viwango vipya vya safari kabla ya kupewa kibali na Msajili wa Hazina.
Aidha,
PAC imemuagiza Msajili wa Hazina kuhakikisha anafanya ukaguzi wa haraka
kuangalia kama viwango kwa ajili ya safari vikoje na kuweka uwiano wa
viwango vya safari kwenye mashirika mengine ya umma.
PAC
pia imemwagiza Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), kufanya
ukaguzi maalumu katika matumizi tata ya Sh bilioni 26.
Matumizi
hayo ni Sh bilioni 9.6 zilizotumika kwenye mkutano moja wa wafanyakazi,
Sh bilioni 6.4 zilizotumika kwa ajili ya matangazo, Sh bilioni 10
zilizotumika kwenye safari na Sh bilioni 43 kwa ajili ya manunuzi ya
dharura.
Kwa
mujibu wa agizo la PAC, wafanyakazi hao watalazimika kulipa fedha hizo
kuanzia mwaka 2011 hadi Januari Mosi, mwaka huu, yaani siku moja kabla
Msajili wa Hazina hajatoa kibali kubariki posho mpya Januari 2 mwaka
huu.
Menejimenti
na Bodi ilipitisha viwango vya safari ambavyo ni Sh 500,000 kwa kada ya
juu na Sh 125,000 kwa kada ya chini na ambavyo TPA walianza kuvitumia
bila kupewa kibali tangu mwaka 2011 hadi Januari 1 mwaka huu. Viwango
vya awali vilikuwa ni Sh 270,000 kwa ngazi ya juu na Sh 94,000 kwa kada
ya chini.
“Ninawaagiza
kuhakikisha wale wote walionufaika na viwango vipya vya safari kabla ya
vibali kutolewa, kuhakikisha wanarudisha fedha hizo za umma, mtatafuta
njia ya kuhakikisha wafanyakazi hao wanarejesha na hata kama ni kukatwa
kwenye mishahara,” alisema.
Aidha,
Zitto alisema: “ Nifikishieni salamu kwa (Lawrence) Mafuru (Msajili wa
Hazina) kuhakikisha mnafanya ukaguzi wa haraka kwenye mashirika mengine
kama Ewura, LAPF, NSSF na mengine kuangalia viwango vya safari
wanavyolipana na ili kuweka usawa na kwenye mashirika.”
Aidha,
Menejimenti ya TPA ililiambia Bunge kuwa watahakikisha mamlaka inatumia
mfumo wa kisasa katika mahesabu na shughuli nyingine.
“Tulikuwa
tunatumia mfumo wa kizamani ambao ulikuwa na matatizo lakini sasa
tunataka kununua mfumo mpya wa ERP ambao pia hutumiwa na hata bandari za
nchi zingine,” alisema Meneja wa Tehama, Phares Magesa.
Hatua
hiyo ya kutaka kufungwa kwa mfumo wa kisasa wa kielektroniki katika
hesabu na shughuli za bandari, unatokana na ripoti ya CAG kubainisha
kutokuwapo kwa nyaraka zinazothibitisha matumizi kutokana na mahesabu
kufanywa kwa mkono.
Katika
ripoti hiyo, kwenye fedha zilizotumiwa kwa ajili ya mikutano ya
wafanyakazi, zaidi ya Sh bilioni 600 hazina nyaraka ya matumizi yake na
kwenye hoja ya matumizi ya matangazo Sh milioni 384 zimekosa nyaraka za
matumizi yake.
Aidha,
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Madeni Kipande alisema uongozi wake
umeweza kubadilisha sheria ambazo zilikuwa zikitoa mwanya kwa mkurugenzi
kuidhinisha fedha zaidi ya bajeti na kwa kufanya hivyo, wameweza
kupunguza matumizi kwa asilimia 30