UCHAFU WATAWALA USIKU WA MKESHA MWAKA MPYA
HII
kweli ni aibu funga mwaka! Msanii wa Bongo Movies, Stani Bakora
amenaswa na paparazi wetu akivunja amri ya sita ndani ya gari na dada
mmoja ambaye jina lake halikupatikana mara moja, Amani linakupa mchapo
kamili.
Tukio
hilo la kinyaa lilitokea hivi karibuni maeneo ya Masaki jijini Dar es
Salaam, karibu kabisa na maegesho ya magari yanayotumiwa na ukumbi wa
burudani wa New Maisha.Chanzo makini kilichomuona msanii huyo,
kilimtonya paparazi wetu siku hiyo baada ya kubaini msanii huyo amekuwa
na kamchezo hako kachafu kila anapokwenda klabu hapo.
“Huyu
jamaa amekuwa na haka kamchezo ka kwenda kumalizia kwenye parking za
magari sasa leo kaja na kabinti f’lani hivi, njooni mmnase,” kilisema
chanzo hicho.Bila kupoteza muda, paparazi wetu alitumia usafiri wa
bodaboda ndani ya dakika sifuri alifika eneo la tukio ambapo siku hiyo
kwenye ukumbi wa New Maisha Club kulikuwa kuna shoo ya Bunyerobunyero
iliyokuwa na watu wachache.
Paparazi
wetu alimkuta Stan akiwa nje ya gari aina ya Toyota Altezza akivutana
kimahaba na mrembo huyo huku wakibusiana na muda mfupi baadaye walizama
ndani ya gari hilo ndipo paparazi wetu alipoitendea haki kamera yake kwa
kufotoa picha kadhaa.
Stan
na mrembo huyo baada ya kushtuka na kuona mwanga wa kamera ukiwawakia
kama taa za gari, walikurupuka na kuanza kumpiga mkwara paparazi wetu
ambaye alisimamia kazi yake kikamilifu ndipo mrembo huyo aliyekuwa
ametinga kigauni kifupi cheusi alipotimua mbio baadaye Stan naye
akamfuata na kutokomea.