SOMA KICHEKESHO HIKI UJUE KUWA DUNIANI KUNA WATU WENYE AKILI SANAAAAAAAAA


 Dogo mmoja anasoma darasa la tatu.
Dogo:mwalimu mimi nataka kusoma darasa
la nne maana hili la tatu halinifai,nina akili
sana
Mwalimu:mmh hebu nikuulize maswali
Dogo:sawa
Mwalimu:kwenye ndege kuna matofali 20
ukidondosha moja chini yanabaki mangapi?
Dogo:hili swali rahisi mno,yatabaki 19
Mwalimu:nipe hatua za kumweka tembo
kwenye fridge
Dogo:unafungua fridge,unamuingiza tembo
kisha unafunga friji
Mwalimu:nipe hatua za kumweka nyani
kwenye fridge
Dogo:unafungua fridge na kumtoa huyo
tembo uliyemweka kwanza kisha unamuingiza
nyani
Mwalimu:simba anasherehekea siku yake ya
kuzaliwa,wanyama wote wapo kasoro mmoja
tu, Ni nani na kwa nini?
Dogo:ni nyani kwa sababu tumemuweka
kwenye fridge
Mwalimu:bibi kizee amevuka mto wenye
mamba na viboko wengi,aliwezaje?
Dogo:amevuka kwa sababu wanyama wote
walikuwa kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa
ya simba
Mwalimu:sawa,ingawa bibi alivuka
mto,mwishowe alifariki,unadhani kwa nin?
Dogo:alikufa kwa kudondokewa na tofali
kutokakwenye ndege,kwenye yale 20
_____________________________________________
 Nani mtani jembe? Nyumba ya mlevi mmoja nje kuna shimo kubwa la maji bila mfuniko. Siku moja karudi usiku kalewa tooooop, mambo yakawa hivi:
MUME: Fungua mlango!
MKE: Leo sifungui! Nimechoshwa na ulevi wako.
MUME: kama hufungui najitupa kwenye hili shimo nife kabisa.
MKE. Kufa huna faida yoyote duniani!
MUME kachukua jiwe kubwa kalitupa kwenye shimo dubwi!
MKE kajifunga kanga, kafungua mlango. Ghafla mume kaingia ndani na kumfungia mke nje.
MKE: Nifungulie la sivyo nitapiga kelele majirani waje.
MUME: Piga kelele na wakija uwambie unatoka wapi usiku huu na khanga moja. Nan jembe hapo, mume au mke?
Jamaa mmoja alikuwa anasumbuliwa na panya nyumbani kwake siku moja  akaamua kuwategea sumu kwa kuipaka kwenye kiti moto(nyama ya nguruwe), kesho yake alipoangalia mtego akakuta kuna kikaratasi kmeandikwa.... “Utuwekee kwenye samaki sisi wengine waislam!!”
_________________________________________________

Mke: Mme wangu hapo kwa jirani kuna sherehe ya nini tena,nasikia shamra shamra
Mme: Hata sijui ni sherehe ya nini labda ni happy birthday
Mke: Happy birthay ya nani?
Mme: Itakua ya Tuyu,nimesikia wanaimba happy birthday tuyu
_______________________________________
Machizi wamekaa sehemu mara ghafla ikapita ndege angani.
Chizi wa kwanza akasema:ndege ile itakua imembeba raisi.
Chizi mwenzie akajibu:hapana imebeba wazungu kama ingembeba raisi tungeona pikipiki zimetangulia mbele...
da!balaaa
_______________________________________
Mke:Hivi mume wangu nikifa utaowa tena?
Mume:Ndio ntaoa

Mke:ukioa huyo mwanamke ataishi humu?
Mume:Ndio ndani

Mke:Huyo mwanamke atalala kwenye kitanda hiki?
Mume:Ndiyo kitanda kitadumu sana hiki,

Mke:Vip atavaa hadi nguo zangu?
Mme:Hilo sina uhakika kwani yeye mnene kidogo
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.