PENNY ALILIA MIMBA ALIYOTOA BAADA YA KUKAA MDA MREFU BILA MTOTO
PENNY UNATAKA MTOTO SAWA, UNAKUMBUKA MADUDU ULIYOYAFANYA NYUMA?
Binafsi
mimi ni mzima wa afya, namshukuru Mungu hakuchi kunakucha.
Naendelea na majukumu yangu ya kila siku maana kazi yangu
mimi ni kama ya madaktari, haina cha sikukuu, nitalala uzeeni
lakini sa hivi acha niendelee kusaka matukio na kuwajuza
Watanzania.
Madhumuni
ya kukukumbuka leo katika safu hii ya Barua Nzito ni kutaka
kukukumbusha kwamba unapaswa kuwa makini katika nyendo zako.
Maisha huwa hayajaribiwi, yakishapita ndiyo yamepita.
Binadamu tuna uhakika wa maisha ya leo, yajayo hatuyajui.
Juzi
kupitia baadhi ya magazeti niliona habari juu ya wewe
kutamani mtoto. Kimsingi nilipenda na kuona kwamba una nia ya
dhati kumpata. Pamoja na nia yako hiyo nzuri, nilipata shaka
kidogo kama kauli yako hiyo ulikuwa unamaanisha au ulitamka
tu ili mradi kwani kumbukumbu inaonesha uliwahi kupata
ujauzito na kwa sababu ambazo hazieleweki, mimba zikayeyuka.
Kudhihirisha
hilo nilisemalo, ninakumbuka maneno ya aliyekuwa mpenzi
wako, Nasibu Abdul 'Diamond' aliyoyazungumza hivi karibuni
kupitia Global TV Online.
Alifunguka mengi kuonesha hisia zake juu ya suala la kutamani kupata mtoto lakini kimsingi, aliumia kwa kile alichosema kwamba ulimfanyia ujanjaujanja na akajikuta amepoteza kiumbe ambacho alikuwa na imani kwamba utamzalia.
Alifunguka mengi kuonesha hisia zake juu ya suala la kutamani kupata mtoto lakini kimsingi, aliumia kwa kile alichosema kwamba ulimfanyia ujanjaujanja na akajikuta amepoteza kiumbe ambacho alikuwa na imani kwamba utamzalia.
Mbaya
zaidi alidai si mara moja, alisema kutokana na sababu za
nyinyi mabinti wa mjini kupenda kula ujana, wengi wenu huwa
hampendi kuzaa na ndiyo maana hata ilipotokea amekupa mimba
ya pili, nayo ukaitoa pasipo kuwa na sababu za msingi.
Kuonesha msisitizo wa namna ambavyo Diamond aliumia, ngoja nimnukuu hapa:
"Nikampa mimba ya kwanza, sikuamini ikabidi twende naye hadi hospitali, tukapima akaambiwa anayo...nikafurahi nikampiga na ndinga mpya siku hiyohiyo. Nikamwambia mama tulia unizalie mwanangu.
"Nikampa mimba ya kwanza, sikuamini ikabidi twende naye hadi hospitali, tukapima akaambiwa anayo...nikafurahi nikampiga na ndinga mpya siku hiyohiyo. Nikamwambia mama tulia unizalie mwanangu.
"Sikukaa
sana akaniletea maneno oooh mara hivi mara vile, eti imetoka.
Nikasema poa, labda haikuwa riziki. Nikampa ya pili nayo pia
akatoa. Nikasema bora niachane naye. Na huo ndiyo ukawa
mwisho wa mimi na Penny."
Kwa
maneno hayo ya Diamond inaonesha ni dhahiri ulimfanyia
ujanjaujanja ukatoa mimba zake kitu ambacho kinaweza
kukusumbua sana akilini mwako. Kutoa mimba si jambo jema hata
kidogo, ikifanyika vibaya inaweza kukusababishia matatizo
kiafya.
Kwa nini
lakini uliamua kumfanyia kitu kama hicho? Kwa kuwa yaliyopita
si ndwele, tugange yajayo. Nikushauri tu, kwa kuwa kwa sasa
unahitaji mtoto basi tusije tukasikia hadithi kama hizo
tulizosikia. Zaa bwana, wenzio wanawatafuta watoto miaka na
miaka hawawapati.
Kama
haupo tayari kuzaa basi usikubali kupata ujauzito, mimba ni
kitu ambacho kinazuilika. Ni vyema ukajizuia hadi muda ambao
kweli utakuwa tayari.
Kwa leo ngoja niishie hapo, nikutakie kazi njema.
Wako,
Erick Evarist
Wako,
Erick Evarist