MWENYEKITI WA CHADEMA IRINGA MATATANI
| Mwenyekiti wa Chadema Iringa Mjini |
MWENYEKITI
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Iringa Mjini, Frank
Nyalusi ameingia matatani baada ya kudaiwa kutoa tuhuma zisizo za kweli
dhidi ya Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa
wa Iringa, Salim Asas, kwa lengo la kujipatia umaarufu.
Katika
mkutano wa hadhara uliofanywa na Chadema hivikaribuni kwenye uwanja wa
Mwembetogwa mjini Iringa, Nyalusi ambaye pia ni diwani wa kata ya
Mivinjeni mjini Iringa, anadaiwa kutoa tuhuma zinazowahusisha vijana
watatu ambao hata hivyo hakuwataja majina; kwamba walitumwa na Kamanda
huyo wa UVCCM kwenda kumdhuru.
Taarifa
za uhakika zilizoufikia mtandao huu zimedai Asas kwa kupitia wakili
wake, Alfred Kingwe amekwisha mkabidhi Nyalusi hati ya madai (Demand
Note) inayomtaka kukanusha tuhuma hizo ndani ya siku 14 vinginevyo
atafikishwa mahakamani.
Kwa
kupitia hati hiyo ya madai Nyalusi anatakiwa kuitisha mkutano katika
eneo lile lile alilotolea tuhuma hizo na kukanusha madai hayo
yanayoelezwa kupikwa kwa lengo la kuchafua wasifu wa Asas na kumuongezea
Nyalusi umaarufu.
Katika
kumnurusu Nyalusi dhidi ya mkono wa sheria endapo atashindwa kuitisha
mkutano huo, baadhi ya viongozi wa chama hicho wanadaiwa kumpigia magoti
Bwana Asas ili suala hilo limalizwe kiungwana.
Mmoja
wa viongozi wa chama hicho, Abou Changawa alisema; “tunamtafuta Bwana
Salim, tunajua ni muungwana, tunataka suala hili tulimaze kiungwana;
kama itashindikana kuitisha mkutano wa hadhara basi tutafanya mkutano na
waandishi wa habari ili kuiweka sawa taarifa hiyo.”
Mtandao huu utaendelea kukujuza kinachoendelea kuhusiana na habari hii.....
CHANZO:BONGO LEAKS