AJALI MBAYA YATOKEA IRINGA YAFUNGA BARABARA USAFIRI NI SHIDA
Watumiaji
wa barabara ya Iringa Njombe wamekwama toka jana majira ya saa 10 jioni
kufuatia ajali ya lori lililobeba shaba lenye namba za usajili T 261
BCM linalovuta tela lenye namba za usajili T 595 BAS kupata ajali na
kufunga barabara na kusababisha magari kushindwa kupita.
Mtandao
huu umeshuhudia msururu mkubwa wa magari yanayokwenda mikoa ya njombe
Ruvuma Mbeya na nchi jirani, pamoja na yanayotoka kwenye mikoa hiyo
kwenda Iringa Dodoma, Dare es Salaam na mikoa mingine yakiwa yamekwama
kwenye msururu huo.
Ajali
hiyo imetokea eneo la Nyororo mkoani Iringa. Baadhi ya abiria na
madereva wa malori waliokuwa eneo la tukio wamelalamikia ufinyu vya
kulitoa lori hilo kuwa ni hafifu hali iliyopelekea wakae hapo muda
mrefu(karibia siku moja).
Hali
hiyo iliondolewa majira ya saa tatu asubuhi baada ya lori hilo
kufanikiwa kuondolewa barabarani na kusogezwa pembeni ndipo magari hayo
yakaendelea na safari. (na Edwin Moshi wa Eddy Blog)












