MAKADA WA CCM WAFIKISHANA MAHAKAMANI HUKO MOSHI: NINI MTAZAMO WAKO JUU YA CHAMA HIKI?




Katibu Mwenezi WA ccm kata ya Uru kusini jimbo la Moshi vijijini Dominick Mbararia amepandishwa kizimbani Leo mjini Moshi akituhumiwa kumtukana na kumtishia maisha kada mwenzake Mkiti mstaafu WA ccm kata gamba Dennis Safisha.Ugomvi huo ulitokana na kutuhumiana kukisaliti chama ambapo katika kata hiyo yenye vijiji saba ccm imeambulia kijiji kimoja na CHADEMA kuzoa vijiji sita.

Hata hivyo mtuhumiwa amekana shtaka na ameachiwa kwa dhamana.Gamba huyo amesikika akisema kamwe hakukisaliti chama Bali matokeo ya uchaguzi huo ni mabaya kwa ccm MKOA mzima WA Kilimanjaro na kwamba hayo ndiyo maamuzi ya wananchi.Aliongeza kwamba yeye alipangiwa kampeni kijiji cha Rau na walifanikiwa kushinda na kuwashangaa magamba wenzake kwa kumtuhumu wakati wao hawakushinda kwenye vijiji walivyopangiwa.
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.