INASIKITISHA SANA MTOTO WA MIAKA 15 AKUTWA AMEFARIKI: TAZAMA PICHA ZAKE HAPA

MWANAFUNZI
wa kidato cha kwanza katika shule ya Sekondari Kambangwa,Denis Casmiry
mwenye umri wa miaka 16 (pichani) amekutwa kwenye ufukwe wa Salander
Bridge akiwa amefariki dunia
Akizungumza
na Ripota wetu huku akionekana kuwa na masikitiko makubwa,Baba Mzazi wa
Mtoto huyo aliejitambulisha kwa jina la Casmiry,amesema kuwa walipata
taarifa ya mtoto wao kupotea toka Jumamosi Desemba 20,2014 ambapo
inadaiwa kuwa aliondoka nyumbani kwao akiwa na marafiki zake kwenda
kwenye Mazoezi ya viungo kwenye ufukwe huo wa Coco Beach.
"Aliondoka
hapa nyumbani asubuhi na mapema kwenda kwenye mazoezi akiwa na
wenzake,na walipomaliza kufanya mazoezi yao hayo,waliamua kuogelea
kidogo ikiwa ni kawaida yao kila wanapomaliza mazoezi wanafanya
hivyo,mara baada ya kumaliza kuogolea wenzake walitoka kwenye maji na
hapo ndipo walipobaini kuwa mwenzao hawakuwa nae" alisema Bw. Casmiry.
Aliendelea
kusema kuwa "Baada ya kufanya juhudi za kumtafuta mwenzao bila
mafanikio,vijana hao walirudi nyumbani na kutupatia taarifa na sisi bila
kuchelewa tulitoa taarifa kituo cha Polisi na kutoa na askari wachache
mpaka eneo la tukio na pia hatukuweza kumuona mpaka leo hii tunaukuta
mwili wake Ufukweni,inauma sana kwa kweli".
Mwili ya kijana huyo umekutwa kwenye ufukwe ya Salander Bridge,Jijini Dar es Salaam leo.
Sehemu ya ndugu wa kijana huyo pamoja na Askari Polisi wakiwa wameubeba mwili wa kijana huyo.
Askari
Polisi waliokuwepo kwenye eneo la tukio wakijadiliana jambo wakati
wakijiandaa kwenda kuuhifadhi mwili wa kijana huyo kwenye Hospitali ya
Taifa Muhimbili,jijini Dar es Salaam.

