Wabunge wavurugwa mkopo magari mil.90/-
Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamegawanyika kwa kiasi kikubwa kuhusiana na Sh. milioni 90 za mikopo ya magari walizoanza kulipwa mwishoni mwa wiki.
Baadhi yao wameafiki kwa shingo upande huku wengine wakipinga kwa maelezo kuwa fedha hizo haziendani na bei ya soko ya magari yanayoweza kuhimili changamoto za miundombinu ya barabara kwenye majimbo yao.
Nipashe ilithibitishiwa kuwa kuanzia juzi, wabunge walianza kuingiziwa fedha hizo kwenye akaunti zao huku baadhi wakikiri kukuta kiasi hicho badala ya Sh. milioni 130 kilichokuwa kikitarajiwa na wengi wao.
Kundi la kwanza lililojumuisha wabunge 160 ndilo lililoingiziwa fedha hizo juzi akiwamo Mbunge wa Donge (CCM), Juma Sadifa, aliyekiri kuingiziwa Sh. milioni 90 lakini akakuta Sh. milioni 89, kiasi kingine kikikatwa kwa ajili ya gharama za bima. Wengine wanatarajiwa kupata fedha hizo kati ya leo na kesho.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Nipashe jana, baadhi ya wabunge walisema kiasi hicho hakitoshi kwa kuwa kimetokana na makadirio ya mwaka 2010 wakati wa Bunge la 10 na kwamba hivi sasa fedha hizo hazina nguvu ya kununulia magari madhubuti ya kuwasaidia katika kutekeleza majukumu yao majimboni.
Aidha, wapo wabunge waliokiri kwamba kiasi hicho ni kidogo, lakini wanaridhika nacho ili kuipa unafuu Serikali ya Rais Dk. John Magufuli katika kutimiza dhamira yake ya kutatua kero mbalimbali za wananchi, hasa zinazohusiana na huduma za kijamii kama maji na utoaji wa elimu bure.
Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa, alisema wanacholalamikia kuhusiana na mkopo huo ni kupewa fedha kwa kuzingatia bei ya zamani ya gari madhubuti aina ya Toyota Land Cruiser, ambalo wakati wa kuanza kwa Bunge la 10 mwaka 2010 lilikuwa likiuzwa kwa Sh. milioni 90 lakini hivi sasa bei yake imepanda hadi kufikia Sh. milioni 150.
Aliongeza kuwa mazingira ya majimbo yao nchini yanatofautiana, hivyo hata mahitaji ya magari kwa wabunge hutofautiana, akitolea mfano wa jimbo lake kuwa ni dogo na lina miundombinu mizuri, tofauti na wenzake wengi wa majimbo ya vijijini.
Alisema kuna majimbo yanahitaji magari imara kama ya aina ya Land Cruiser Hardtop maarufu kama ‘mkonge’, ambalo jipya huuzwa kuanzia Sh. milioni 150 hivyo wanapaswa kupewa fedha zitakazotosha kununua magari ya aina hiyo ili kuwaondolea bughudha ya usafiri wabunge waishio kwenye majimbo yenye miundombinu duni ya barabara.
“Kwa sababu hiyo, fedha hizi zinaweza kuwa kidogo au nyingi kwa mbunge kulingana na ukubwa wa jimbo lake na miundombinu ya jimbo husika,” alisema Msigwa.
Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Keissy Mohamed, alisema fedha hizo (Sh. milioni 90) hazitoshi kununulia gari litakalokidhi mahitaji yake katika kuwatembelea wananchi wa jimbo lake.
Alisema jimbo lake lina ukubwa wa mita za mraba 8,000 na miundombinu yake ni mibovu, hivyo anahitaji gari imara litakaloendana na mazingira ya jimbo lake.
“Kuna majimbo unaweza kutumia bajaji kutembelea au hata kusafiri kwa miguu lakini si jimbo la kwangu. Mbuga ya wanyama peke yake ina mita za mraba 2,000. Fedha hizi hazitoshi,” alisema Keissy.
Hata hivyo, alisema hajapata fedha hizo, lakini atakapozitia mkononi ataongezea fedha zingine ili kununua gari imara.
Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM), Steven Ngonyani, alisema kutokana na hali ya kiuchumi, wabunge wanapaswa kukubalina na mkopo huo wa Sh. milioni 90 hata kama haukidhi mahitaji yao.
Alisema kwa kufanya hivyo, wabunge wataonyesha kuwajali wananchi wao ambao hivi sasa wengi hupata shida mbalimbali ikiwamo ya uhaba wa dawa hospitalini, hivyo mkopo huo wa gari kama ni mkubwa au mdogo, wanapaswa kuupokea.
“Yaani Mbunge aongezewe fedha za gari wakati wanafunzi wanakaa chini, au hakuna dawa hospitalini…hiyo haitakuwa sawa,” alisema Ngonyani.
Kadhalika, alisema kwa Sh. milioni 90 mbunge anaweza kununua gari zuri la kutembelea jimboni kwake, mfano kuna gari za muundo wa ‘pick up hard board’ ambazo ni imara, nzuri na bei yake huanzia dola za Marekani elfu 50 (Sh. milioni 107) hivyo kazi ya mbunge itakuwa kuongeza kiasi kilichozidi.
Alisema ni kweli wabunge wanahitaji magari kwa ajili ya kufika majimboni kwao ambao wengine miundombinu ni mibovu, lakini kwa sasa wabunge wanapaswa kukubalina na hali iliyopo kwa kupokea kiasi cha fedha walichopewa.
Mbunge wa Urambo (CCM), Margaret Sitta, alisema wabunge kwa sasa wanapaswa kusubiri na kuwa watulivu kama walivyopewa taarifa na Spika wa Bunge.