UKAWA: Deni la Taifa Limefikia Trilioni 41.5
Akiwasilisha maoni ya kambi ya upinzani kuhusu mpango wa serikali wa maendeleo kwa mwaka 2016&2017 msemaji wa kambi hiyo Mbunge wa Momba (CHADEMA) David Silinde amesema serikali imekopa fedha nyingi huku maendeleo na fedha zilizokopwa yakiwa haya endani na miradi iliyotekelezwa.
Mfano katika mpango wa miaka 5 iliyopita serikali iliahidi kupata umeme wa megawati 2780 ambapo kila mwaka ilitakiwa izalishe megawati 556 lakini ilizalisha megawati 344 hii inaashiria kwamba utekelezaji wa miradi haukuenda kulingana na ahadi zilizotolewa.
Aidha kambi ya upinzani bungeni imeitaka serikali kutotegemea zaidi wahisani ila wapange miradi kulingana na vipaumbele maalum ili kuweza kuleta ufanisi.