UCHUMI WA SERIKALI NI MBAYA BAADHI YA SEKTA KUKOSA FEDHA

Uchumi wa serikali siyo imara kiasi cha kuweza kutoa fedha kila sekta.
Serikali imesema bado uchumi wake siyo imara kiasi cha kuweza kutoa fedha za kutosheleza kwa kila sekta kama ilivyoanza kufanya mahakamani bali itahakikisha inakusanya mapato yote na kudhibiti mianya ya upotevu na ubadilifu wa fedhza za umma lengo likiwa ni kuhakisha kuwa kila mtu ananufaika na kidogo kitakachopatikana.
Hayo yamesemwa katika mkutano uliohudhuriwa na waziri wa katiba na sheria Mh Dk Harison Mwakyembe na jaji mkuu Mohamedi Othumani Chande na waziri wa fedha na uchumi Mh Dk Philipo Mpango wakati akithibitisha kuingizwa zaidi ya shilingi bilioni 12 katika akaunti ya mfuko wa mahakama kwa ajili ya kuboresha huduma za mahakama.

Naye waziri Mwakyembe amesema anaimani kuwa fedha hizo zitasaidia kuinua huduma za kimahakma ikiwemo ujenzi wa mahakma mpya ambazo zitasaidia kupatikana kwa haki za watu kwa wakati.

Kwa upande wake jaji mkuu Mh Chande amesema ili kufanikisha kuweza kuondo tatizo la majengo ya mahakama nchini zinahitajika shilingi bilioni 40 kwa kipindi cha miaka minne.
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.