TUNDU LISU AWEKWA MTU KATI BUNGENI
Ni baada ya kuomba Mwongozo kuhusu swala lililoleta utata kwa siku kadha kuhusu uhalali wa serikali kuwasilisha mpango wa mwaka mmoja badala ya miaka mitano.
Awali akiomba Mwongozo mh.Lissu alisema serikali imekiuka kuleta mpango wa mwaka mmoja badala ya miaka mitano ambayo ndio desturi ya mabunge yote yaliyopita na kumtaka Spika kutokubali kuruhusu bunge lake tukufu kukiuka kanuni zake kwa faida ya serikali. Huku akiendelea na kibwagizo cha hapa kazi tu hapa kazi tu.
Kwa kukazia ndipo akasimama Mh.Zitto na kuikumbusha serikali kuwa serikali ilikuwa na uwezo kuwasilisha hoja ili kanuni zitenguliwe na mpango wa mwaka moja ujadiliwe na kanuni zinaruhusu utenguaji huo.
Ndipo aliposimama Waziri na kusema kuhusu suala la utenguaji wa kanuni serikali ilishakaa na kamati ya kanuni ambapo kiongozi wa KUB alishiriki kwa kutuma mwakilishi, na Mwakilishi mwenyewe alikuwa Lissu.
Waziri akasema anamshangaa Lissu kwa kuomba mwongozo jambo ambalo alishiriki kutoa maamuzi na akasema anaweza kutaja hata majina ya wajumbe wote walioshiriki huo uamuzi.
NB. Wabunge waache unafiki na kuwa vigeugeu kwa kutafuta umaarufu usio na tija