TUNDAMAN AAMSHA AKINAMAMA TANDALE DAR!

Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, ambaye pia ni Balozi wa Kampeni ya Amsha Mama 2016 Tundaman (kulia), akiongea jambo na mama Rishe Sophia Amri au maarufu kwa jina la Mama Dayna muda mfupi baada ya kumkabidhi kiasi cha shilingi laki moja ikiwa ni njia mojawapo ya kutekeleza kampeni ya Amsha Mama 2016, aliyoanza kutekeleza majuku yake katika soko la Tandale jijini Dar es Salaam, anayeshuhudia zoezi hilo kushoto kwake ni Mkurugenzi wa kampeni hiyo Joe Kariuki.
Tundaman akiongea jambo na mama huyo baada ya kumaliza kumchangamsha kwa kumpatia kiasi cha shilingi laki moja Antonia Msomboki.
Balozi wa kampeni ya Amsha Mama 2016, Tundaman akichagua nguo moja wapo zilizokuwa zikiuzwa na Mjasiliamali Sakina Thomas, kulia ni Mkurugenzi wa Kampeni hiyo Joe Kariuki.
Balozi wa kampeni ya Amsha Mama 2016, Tundaman (katikati), akimkabidhi kiasi cha shilingi laki moja Antonia Msomboki ambaye ni mfanya biashara wa matunda katika soko la Tandale jijini Dar.
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.