SIMBA SPORT CLUB WAZINDUA DUKA LA VIFAA VYA MICHEZO
Rais wa Simba Sport Club Evans Aveva Akikata Utepe wakati wa Uzinduzi wa Duka la Vifaa vya Michezo akiwa Ameambatana na Afisa Mtendaji Mkuuwa Eaggroup Ndugu Iman Kajula Pamoja na Wadau wengine wa Club Hiyo.
Katika kukuza wigo wake wa mapato pamoja na upatikanaji wa vifaa, klabu ya Simba leo imezindua duka lake rasmi kwa ajili ya kuuza vifaa vya michezo vyenye chapa ya Simba.
Katika kukuza wigo wake wa mapato pamoja na upatikanaji wa vifaa, klabu ya Simba leo imezindua duka lake rasmi kwa ajili ya kuuza vifaa vya michezo vyenye chapa ya Simba.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Rais wa Simba Evans Aveva alisema “kama mtakumbuka moja ya malengo ambayo uongozi wangu huu uliopo madarakani ulijiwekea ni pamoja na kuongeza wigo wa mapato kupitia vyanzo vyake vilivyopo lakini pia kuja na mkakati kabambe kwa ajili ya kuongeza na leo wote tunakuwa mashuhuda katika kuzindua duka letu la vifaa vya michezo. Duka ambalo litakuwa likiuza kila bidhaa ambayo inachapa Simba hivyo wanachama na wapenzi wa Simba kuweza kujua ni wapi mahala pa kupata vitu halisi vya Simba na kwa bei nafuu zaidi”
Duka hili si tu litasaidia katika kuongeza mapato kwa klabu lakini pia litaziba mianya yote ya wale watu wote wasio itakia mema klabu yetu na kuamua kutengeneza vitu feki vyenye chapa ya Simba, kwakuwa sasa mtu ukikutwa na bidhaa feki basi mkono wa sheria utakuwa juu yako. Nipende kuwa sisistiza wanachama, wapenzi na wadau wote wa Simba na soka la Tanzania kwa ujumla kuwa kwanza tupende vyetu vya nyumani lakini pia tupende kutumia vitu halisi na kuachana na utamaduni wa mazoea ya kutojali ni kipi halisi na kipi ni feki” aliongeza Rais Aveva.
Akizungumza kwenye ufunguzi huo Mkurugenzi wa kampuni ya EAG Group Ltd ambao ni washauri na watekelezaji wa masuala ya biashara na masko kwa klabu ya Simba Bw. Imani Kajula alisema “nadhani sasa wanasimba tunaweza kufurahia vya kwetu kwani kwa sasa tunajua ni wapi vinapatikana na ni wapi ukienda huwezi kukutana na kitu feki chenye chapa ya Simba na hapo si pengine bali ni Simba Sports Shop lililopo katika jingo la DarFree Market. Pamoja na kuwepo kwa duka hili lakini pia vifaa vyote vitakavyokuwa vikipatikana hapa ndani ya siku za hivi karibuni vitakuwa vikipatikana kwenye duka mtandao (Online Shops) na hivyo kuweza kuwafikia watu wote popote walipo nchini Tanzania”.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa duka hilo msimamizi wa Duka la vifaa vya michezo venye chapa ya Simba mkurugenzi wa kampuni ya Insight Media Bw. Tahir Othman ambao ni waamiliki wa Dukakwa kuhamasisha wapenzi wote wa Soka Tanzania kuweza kuunga mkono juhudi zinazofanywa na klabu ya Simba ili kuweza kukuza mapato kwa klabu yetu lakini pia kuweza kupata bidhaa bora na halisi za chapa ya Simba.