RUFIJI YAKUMBWA NA MAFURIKO
Zaidi ya wananchi 5000 wa Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani hawana mahali pakuishi baada ya nyumba zao kukumbwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali hapa nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo amesema serikali imekwishachukua hatua za haraka kuwasaidia wananchi hao kwa kutoa tani 1283 za chakula (mahindi) cha dharura.
Ndikilo alisema kuwa mbali na serikali kutoa tani hizo za mahindi pia imetoa mbegu za mahindi tani 10 sambamba na tani 5 za mtama ambazo zinastawi kwa kipindikifupi ili wananchi hao wazipande ukanda wa juu.